WATUMISHI GST WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI KUFIKIA LENGO LA SERIKALI

February 21, 2025


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo leo amefungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) huku akiwawataka watumishi wa wizara hiyo kutimiza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa weledi, ubunifu, uaminifu na ufanisi ili kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu yao.


Ameyasema hayo wakati akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kilichofanyika katika Mkoani Morogoro.

Amesema Baraza la Wafanyakazi ni chombo pekee kinachoweza kuunganisha Menejimenti na Wafanyakazi kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Taasisi ambalo lipo kwa mujibu wa Agizo la Rais Na. 1 la Mwaka 1970 ambalo lina lengo la kuwashirikisha wafanyakazi wa ngazi zote hivyo ni vyema wakatumia vizuri jukwaa hilo .

"Naelewa kuwa Taasisi inatekeleza majukumu muhimu sana ya kutoa huduma za za tafiti za jiosayansi Jiolojia na Utafiti wa Madini kwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini na wananchi kwa lengo la kubaini aina za miamba na madini inayopatikana nchini. Aidha, taasisi hii mdau mkubwa katika kufikia lengo la maono ya 2030 (Vision 2030). Hivyo kupitia baraza hili viongozi wanatakiwa kupata mawazo mapya ya kuboresha utendaji kazi" amesema Mbibo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa GST ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Mussa Budeba amemshukuru Mbibo kwa kushiriki na kulifungua Baraza hilo ambapo ameahidi kuyatekeleza yale yote yaliyoelekezwa na mgeni rasmi na pia amewataka Wajumbe wa Baraza hilo kutoa maoni na michango yao kwa uhuru na uwazi ili kuboresha utendaji kazi wa taasisi.

"Ninaamini wawakilishi wa wafanyakazi katika Baraza hili watapata fursa ya kuchangia mawazo yenye tija yatakayoleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi na kujenga uelewa wa pamoja wa majukumu yenu katika Baraza na kufanya Baraza kuwa sehemu nzuri ya majadiliano kwa ustawi wa Taasisi na Sekta kwa ujumla," amesema Dkt. Budeba amesema.

Katibu Msaidizi wa Baraza hilo Osiah Kajala ambaye pia ni Mchumi Mkuu wa GST amesema lengo la Baraza hilo ni kujadili utekelezaji wa bajeti iliyopita na kupitisha mpango wa bajeti kwa mwaka 2025/2026 kwa kuwahusisha wawakilishi wa Wafanyakazi ili kuongeza ufanisi, uhuru na uwazi pamoja na kujadili masuala mbalimbali hususan maslahi ya Watumishi.

Kwa uapnde wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu Taifa Straton Lufyagila amesema Baraza la Wafanyakazi lipo kwa mujibu wa Sheria ambapo wawakirishi wa Watumishi wa GST watapata fursa ya kutoa maoni kwa lengo la kuboresha ufanisi wa taasisi na kuongeza uwajibikaji wa Watumishi.





Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »