ETDCO YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA ZICA

February 23, 2025


Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme nchini (ETDCO) imebuka mshindi katika kipengele cha Mkandarasi Bora wa Ujenzi wa Miundombinu ya Umeme, katika Tuzo za Zanzibar International Construction Awards (ZICA) zilizofanyika Februari 22, 2025, Zanzibar.


Akizungumza wakati akikabidhi Tuzo kwa Washindi, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, amesema kuwa  sekta ya ujenzi ni msingi mkuu wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku  akiwataka washiriki wote kutumia tuzo hizo kama chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa  bidii ili kufikia viwango vinavyohitajika na kuleta tija kwa Taifa.


Kaimu Meneja Mkuu wa  ETDCO CPA. Sadock Mugendi, ameishukuru ZICA

kwa kutambua mchango wao  katika sekta ya ujenzi wa miundombinu ya umeme nchini, na kuahidi kuendelea kutoa huduma zenye viwango ili kukuza uchumi wa nchi.


"ETDCO tumejipanga kuhakiksha tunaboresha matumizi ya teknolojia kwa kununua mashine za kisasa pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu ili  kufikia viwango vinavyohitajika kimataifa" amesema CPA.  Mugendi


CPA. Mugendi ameeleza kuwa ETDCO ni kampuni iliyopewa  jukumu la kutekeleza miradi ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umeme kupitia wadau mbalimbali ikiwemo TANESCO, REA pamoja na  makampuni binafsi.


Katika Tuzo za  ZICA kilikuwa na washiriki 150 na ETDCO  miongoni mwa washindi 30 waliotunukiwa tuzo hizo kutokana na ufanisi wa kazi pamoja na  juhudi katika kuhakikisha  miundombinu ya usafirishaji  na usambazaji wa  umeme inakuwa bora na salama ili watanzania waweze kupata umeme wa uhakika wakati wote na kupelekea  kuchochea maendeleo ya uchumi kwa wananchi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »