Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga(Mb) ameiongoza Menejimenti ya Wizara ya Nishati kuwasilisha taarifa ya Wizara hiyo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyowasilishwa Bungeni Mwezi Februari 2024
Taarifa hiyo imewasilishwa kwa niaba na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Nishati Petro Lyatuu ambaye amesema taarifa hiyo ni utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya Bunge ambayo Wizara imetoa ufafanuzi wa utekelezaji wake.
Lyatuu amesema Wizara inaishukuru Kamati kwa ushauri, maoni na ushirikiano mkubwa inaoupata kwa lengo la kuimarisha Sekta ya Nishati nchini na kuchochea maendeleo ya Taifa na watu wake.
Amesema Wizara itaendelea kuzingatia kutekeleza maoni na ushauri wa Kamati ili kufikia malengo yanayokusudiwa.
EmoticonEmoticon