Uongozi wa kituo maalum cha kulelea watoto cha Bero Kids (Bero Kids Day Care) kilichopo jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja mgeni rasmi na wahitimu wa mahafali ya pili.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Fatuma Juma akizungumza wakati wa mahafali ya pili ya kituo maalum cha kulelea watoto cha Bero Kids (Bero Kids Day Care) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius Profesa Aldin Mutembei ambaye pia ni Mhadhiri wa Lugha katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) amewashauri wazazi kuendelea kuwapa watoto wao maadili mema.
Mgeni rasmi Mwigizaji Shamsa Ford ambaye aliambatana na mumewe akizungumza machache wakati wa mahafali ya pili ya kituo maalum cha kulelea watoto cha Bero Kids (Bero Kids Day Care) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mwenza wa Bero Kids Day care Dkt. Bertha Mleke amewaomba wazazi kuendelea kuwaamini katika malezi ya watoto wao huku wakiendelea pia kuwa mabalozi wema katika kuwatangaza.
Mgeni rasmi Mwigizaji Shamsa Ford akiwashukuru kwa waliko Wakurugenzi wa Bero Kids Day Care Eng. Constantine Paschal (Kwanza kulia) na Dkt. Bertha Mleke (katikati).
Wafanyakazi wa Bero Kids Day Care wakitambulishwa.
Wahitimu wakifurahi kwa pamoja.
Wafanyakazi wa Bero Kids Day care wakiwapa zawadi Wakurugenzi wao.
Wazazi wa wahitimu wakiwa na watoto wao.
Na Mwandishi Wetu.
Jamii imesisitizwa kuwa ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha watoto wanapata malezi bora na makuzi yenye maadili mema kwa ajili ya kuwaandaa kuwa wanajamii waadilifu.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Fatuma Juma wakati wa mahafali ya pili ya kituo maalum cha kulelea watoto cha BeroKids (BeroKids Day Care) kilichopo jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kuwa malezi bora yanahusisha pia kumpatia mtoto elimu bora.
Bi. Fatuma Juma amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao katika shule zenye mazingira salama, walimu wenye ujuzi, lishe bora na mfumo wa elimu jumuishi unaokataa aina yeyote ya ubaguzi.
Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius Profesa Aldin Mutembei ambaye pia ni Mhadhiri wa Lugha katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) amewashauri wazazi kuendelea kuwapa watoto wao maadili ya Mtanzania ikiwemo kuwafundisha lugha ya Kiswahili sanifu ambayo kwa sasa imekuwa ikisahaulika kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia zinazoingia nchini.
"Ni muhimu kuwekeza katika maadili mema, ni vizuri kuwalea watoto katika muelekeo mwema ili kupata msingi wa Taifa bora la sasa na baadae. Tuwafundishe watoto wetu lugha za kigeni ila tusisahau mila na desturi zetu", amesema Profesa Mutembei.
Awali akiwakaribisha wageni Mkurugenzi wa Bero Kids Daycare, Eng. Constantine Paschal amesema kuwa shule yao inaendeshwa kwa mfumo wa kingereza (English Medium school) huku ikiwa na vifaa vya kisasa na mazingira salama hivyo huwafanya watoto wanaohitimu kuwa na maadili mema na uelewa mzuri wa lugha ya kingereza na kiswahili japo huko mbeleni wanajipanga kuongeza lugha zaidi kama vile Kichina ama Kifaransa ili waendane na mtaala mpya.
Pia Eng. Constantine Paschal amesema kuwa ni vyema wazazi wakajitoa kuwajengea msingi bora watoto wao ili wanapoanza masomo yao ya awali waweze kufaulu vizuri.
"Niwashauri wazazi kuacha kuwapeleka watoto wao bora shule maana hapa awali ndipo msingi bora wa kumjenga mtoto unapoanzia... kufanya hivyo tutaweza kupata wasomo wenye weledi", amesema Eng. Constantine.
Kwa upande wake Mgeni rasmi Mwigizaji Shamsa Ford ambaye aliambatana na mumewe aliwaomba wazazi waendelee kuwalinda watoto wao dhidi ya watu wanaoweza kuwapotezea ndoto zao katika maisha.
"Jambo langu kubwa ninalowaomba wazazi ni kuhusu kuendelea kuwalinda watoto dhidi ya watu wabaya ambapo wakati mwingine ni ndugu zetu ambao wanatuzunguka hivyo ni vyema kuwa makini," amesema Shamsa Ford.
"Mahafali ya pili yamekuwa ya mafanikio zaidi kwani tumeona muitikio mkubwa kwa wazazi na walezi kuja kujumuika nasi hili kwetu tunaliona ni jambo jema japo niwaombe wazazi wazidi kutuunga mkono kutuletea watoto wengi zaidi kwa muhula ujao wa 2025", amesema Eng. Constantine.
Nae Mkurugenzi mwenza wa BeroKids Daycare Dkt. Bertha Mleke amewaomba wazazi kuendelea kuwaamini katika malezi ya watoto wao huku wakiendelea pia kuwa mabalozi wema katika kuwatangaza.
Ameongeza kuwa nguzo imara wanayojivunia ni kuwa na wafanyakazi bora wenye maadili na Upendo kwa watoto jambo linalofanya shule kuongeza idadi wa watoto kila uchwao.
"Kuendelea kukuwa kwa Berokids shule yetu imefanikiwa kutoa huduma ya kusomesha watoto walio katika mazingira magumu, na kuwagharamikia mahitaji yote ya msingi , sio jambo rahisi, ila tunamshukuru Mungu kwa kutufikisha hapa", Dkt. Mleke.
HISTORIA FUPI YA BEROKIDS DAY CARE;
Berokids day care ilianzishwa mwaka 2022 mwezi wa tisa, na kusajiliwa mwaka huohuo na kupewa namba 2456, ikiwa na jumla ya wanafunzi kumi, sita wa kike, na wane wa kiume, kufikia mwaka 2023 tulibahatika kuwa na jumla ya wanafunzi 33 katika ngazi zote baby, middle, na pre-unit, katika yao waliohitimu ni wanafunzi watano, kwa mwaka huu 2024 shule ina wanafunzi 42, aidha wanaohitimu ni wanafunzi saba, wa kike watano na wa kiume wawili, wapo vizuri, kuanza darasa kwanza kwenye sule mbalimbali ifikapo 2025.
Bero Kids Day Care inapatika Sinza, Bamaga jijini Dar es Salaam ...wasiliana nasi 0766214840. Karibu tukulele mwanao katika misingi ya maadili bora.
EmoticonEmoticon