Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zungu wakiingia ukumbini katika harambee aliyoongoza kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku jijini Dar es Salaam.
|
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na sehemu ya timu ya wataalamu iliyoongozwa na Prof. David Mwakyusa (wa tatu toka kushoto nyuma), ambaye akiwa Waziri wa Afya, yeye Profesa Mohamed Janabi (hayupo pichani) na timu hiyo walitoa mchango mkubwa katika kuanzishwa kwa Taasisi ya JKCI mwaka 2015. |
|
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zung na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jaffo akitoa cheti cha shukurani kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB kwa mchango wao wa shilingi bilioni moja katika harambee ya kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku jijini Dar es Salaam. |
|
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zung na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jaffo akitoa cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Insurance Company Bw. wilson Mzava kwa mchango wao wa zaidi ya shilingi milioni 700 katika harambee ya kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku jijini Dar es Salaam. |
|
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zung na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jaffo akitoa cheti cha shukurani kwa mwakilishi wa taasisi ya kimataifa ya BAPS Charities tawi la Tanzania kwa mchango wake wa dola za Kimarekani laki nne (takriban shilingi 1,078,674,800) katika harambee ya kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku jijini Dar es Salaam. |
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zung na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jaffo akipokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila zawadi ya picha ya kuchora ikimuonesha akimpa pole mtoto wa kwanza kufanyiwa upasuaji wa moyo wakati huo huduma zikipatikana MOI katika harambee ya kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau waliohudhuria katika harambee aliyoongoza Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku jijini Dar es Salaam
Na Issa
Michuzi
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa
wito kwa taasisi na watu binafsi wenye nia njema kujitokeza na kuchangia
matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo ili kuwaondolea
au kupunguza mateso yanayosababishwa na maradhi hayo.
Dkt.
Kikwete alitoa wito huo Jumamosi usiku wakati wa harambee aliyoongoza kuchangia
gharama za matibabu ya watoto hao, iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika
hoteli ya Joihari Rotana, jijini Dar es Salaam.
Rais
Mstaafu, ambaye ni mlezi wa watoto wanaohitaji matibabu ya moyo, alieleza kuwa
lengo kuu la harambee hiyo ni kuchangisha asilimia 30 ya gharama zilizobaki za
matibabu, kwani asilimia 70 ya gharama hizo huchangiwa kila mwaka na Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan.
"Naishukuru
serikali kwa kuchangia asilimia 70 ya gharama zote za matibabu ya wagonjwa hao.
Hata hivyo, asilimia 30 iliyobaki, ambayo familia ya mgonjwa inapaswa
kuchangia, bado ni mzigo mzito kwa familia nyingi. Wanahitaji kusaidiwa,"
alisema.
Alieleza
kuwa kuna watoto 1,500 kutoka familia zisizo na uwezo ambao wamesajiliwa JKCI
wakisubiri matibabu ya haraka ili kuokoa maisha yao. Bila matibabu hayo, watoto
hawa wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupoteza maisha.
"Nawashukuru
sana wadau wote waliochangia katika harambee hii ambapo hadi sasa kiasi cha
shilingi 2,718,525,000/= kimepatikana. Kiasi hiki kitawezesha kugharamia
matibabu ya watoto 500 ambao wanahitaji huduma ya haraka," aliongeza Rais
Mstaafu.
Akitoa
shukurani za pekee kwa Benki ya NMB kwa mchango wake wa shilingi bilioni moja,
aliomba taasisi zingine ziige mfano huu si tu kwa kuwasaidia wagonjwa, bali pia
kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kupunguza au
kutatua tatizo hilo.
Pia
aliipongeza na kuishukuru taasisi ya kimataifa ya BAPS Charities tawi la
Tanzania kwa mchango wake wa dola za Kimarekani laki nne (takriban shilingi
1,078,674,800), pamoja na Benki ya CRDB
kwa kuchangia zaidi ya shilingi milioni 700 katika vipindi tofauti huku
ikiahidi kuendelea na zoezi hilo kila mwaka.
Rais
Mstaafu aliwashukuru pia wadau wote waliojitokeza kwenye hafla hiyo kwa
kuchangia pesa na wengine kutoa ahadi, akiwaomba kila mmoja wao kuheshimu ahadi
aliyotoa ili kufanikisha zoezi zima la kuwaokoa watoto hao wenye matatizo ya
moyo.
Dkt.
Kikwete pia aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na ya Sita kwa kuendelea
kuwekeza kwenye vifaa vya kisasa katika JKCI na kuleta madaktari bingwa, jambo
ambalo limeiongezea uwezo JKCI wa kuhudumia Watanzania wenye maradhi ya moyo.
Alitumia
hafla hiyo pia kumtambulisha Prof. David Mwakyusa, ambaye alisema akiwa Waziri
wa Afya, yeye na timu yake ya wataalamu aliyoiongoza walitoa mchango mkubwa
katika kuanzishwa kwa Taasisi ya JKCI mwaka 2015.
Mwenyekiti
wa HTAF, Mhe. Mussa Hassan Zungu, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, amemshukuru Rais Mstaafu kwa kubuni na hatimaye
kuanzisha Taasisi ya JKCI, ambayo kwa sasa ni ya tatu kwa ubora barani Afrika,
ikifuatia kwa karibu taasisi kama hizo za Misri na Afrika Kusini.
Mhe. Zungu
alieleza kuwa uwepo wa JKCI umepunguza kwa kiwango kikubwa gharama za matibabu
ya wagonjwa wa moyo, kwani uwepo wa taasisi hiyo umewezesha matibabu yaliyokuwa
yakipatikana India na nchi zingine kwa gharama kubwa, sasa kupatikana hapa
nchini na kwa ubora uleule wa huduma za nje.
Mkurugenzi
Mtendaji wa JKCI katika risala yake alisema hivi sasa taasisi hiyo imefikisha
uwezo wake wa kutoa huduma kwa kiwango cha asilimia 90, na kwamba ina madaktari
bingwa wazawa 50 na wa kawaida zaidi ya 40 wanaotoa huduma za kisasa.
Hivi
karibuni, JKCI imepokea tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango mkubwa na wa
kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka
2023/2024.
Tuzo hiyo
ilitolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akifungua kikao kazi cha
wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi za umma kilichoandaliwa na
Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Arusha (AICC).
Tuzo hiyo
inatoa heshima kwa JKCI kwa hatua zake za kufanikisha malengo ya taasisi na
kusaidia taasisi zingine kuweza kufikia mafanikio sawa katika utoaji wa
matibabu ya moyo.
Mafanikio
haya yanaonesha kazi nzuri ya Taasisi hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja
uliopita ambapo JKCI ilitoa huduma za upasuaji mkubwa wa moyo wa kufungua kifua
kwa wagonjwa 654, ambao hapo awali walihitajika kwenda nje ya nchi kwa
matibabu.
Kupitia
upasuaji huo, JKCI imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 9.8 za Kitanzania kutokana
na huduma hizi kupatikana ndani ya nchi.
JKCI pia
imezijengea uwezo nchi za jirani katika kutoa huduma na matibabu ya magonjwa ya
moyo, ikiwemo Hospitali ya Moyo ya Zambia, Hospitali ya King Faisal ya Rwanda,
Hospitali ya Queen Elizabeth ya Malawi, pamoja na hospitali mbalimbali za hapa
nchini.
Share this
EmoticonEmoticon