Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb.) ameshiriki kwenye Kongamano la Biashara na Uwekezaji la Zanzibar na Ubelgiji lililofanyika tarehe 28 Novemba, 2024, Zanzibar na kufunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe. Sharifa A. Shariff.
Kongamano hilo limewakutanisha Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Zanzibar na Ubelgiji Kwa lengo la kujadiliana namna bora ya kuendelea kushirikiana ili kukuza biashara zaidi.
Waziri Shariff amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji hao akiwaahidi kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itashirikiana nao ili kutimiza malengo yao kwakuwa Zanzibar ina fursa nyingi ambazo hazijatumika ipasavyo hivyo ni wakati mwafaka na kuongeza ushirikiano katika maeneo hayo.
Naye, Mhe. Chumi aliwashukuru wafanyabiashara na wawekezaji hao kuja kuitembelea Tanzania na Zanzibar na kuahidi kuendelea kushirikiana nao ili kuwawezesha kuwekeza nchini. Aliwasihi kutembelea mikoa mingine ya Zanzibar kadri ratiba zao zitakavyoruhusu ili kuona maeneo mengine wanayoweza kuwekeza.
Wafanyabiashara hao walitembelea pia
eneo la ujenzi wa Bandari ya Mangapwani na wapo nchini Tanzania tangu tarehe 25 Novemba 2024 ambapo baada ya Kongamano hilo wanatarajia pia kuonana na viongozi mbalimbali wa Wafanyabiashara na Serikali kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam na Zanzibar.
EmoticonEmoticon