Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro Kilahala, kuwasilisha Ofisini kwake orodha ya Taasisi zote za Serikali zinazodaiwa na Wakala huo ili aweze kuwaandikia baraua ya kusisitiza kulipa madeni yao.
Agizo hilo amelitoa leo, Agosti 20, 2024 jijini Arusha wakati akifungua kongamano la Tatu la madereva wa Serikali ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza Wakuu wa Taasisi kuhakikisha wanalipa madeni hayo mara moja ili TEMESA iweze kuhakikisha wajibu wa vyombo vya usafiri vinakuwa salama na vinatengenezwa kwa wakati.
“Wakuu wa Taasisi, popote mlipo mnanisikia, kama mpo hapa ndani au kupitia vyombo vya habari, hakikisheni mnalipa madeni yenu TEMESA, mkiwalipa hawa matengenezo ya magari yenu yatafanyika kwa muda sahihi” amesema Majaliwa.
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa ameipongeza TEMESA kwa kuwa na mitambo ya kisasa ya kutengeneza magari na kuwataka kuongeza ubunifu na uadilifu ili kuleta tija katika utengenezaji wa magari ya Serikali.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka viongozi kuthamini kada ya madereva kwa kuwapa mahitaji yao ili wafanye kazi kwa ufanisi na hivyo kulinda usalama wa viongozi, wananchi na magari wanayoyaendesha.
Ameongeza kuwa Serikali inatambua, inaheshimu na kuthamini mchango wa madereva nchini na itaendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto za madereva ili kuikuza kada hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Naye Naibu waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amemhakikishia Waziri Mkuu kuwa Wizara itaendelea kusimamia na kukilea chama cha madereva ili kikue na kufanya kazi kwa weledi.
"Wizara itahakikisha madereva wanapata elimu stahiki ya magari wanayoyaendesha ili kuendelea na ukuaji wa teknolojia na kuwawezesha kushiriki vikao vyao ili kukuza weledi.
Zaidi ya madereva 1200 kutoka Tanzania bara na Zanzibar wanashiriki kongamano hilo linaloongozwa na kauli mbiu isemayo " Dereva wa Serikali jitambue, timiza wajibu wako, usalama barabarani unaanza na wewe kazi iendelee".
Share this
Related Posts
KAMATI YA BUNGE UJENZI WA BARABARA YA TANGA-PANGANI BAGAMOYO UENDELEE KUPITIA ENEO LA HIFADHI YA TAIFA YA SAADANINa Oscar Assenga, PANGANI KAMATI ya Kudumu ya Bunge Miundombinu imeshauri Serikali ujenzi wa barabara ya kutoka Tanga-P
WANANCHI NJOMBE WAIOMBA TANESCO, REA KUONGEZA KASI YA KUWAUNGANISHIA UMEME Wananchi wa Mkoa wa Njombe ambao bado hawajafikiwa na huduma ya umeme wameiomba Serikali kupitia Shirika la Umeme
TCAA YAJENGA MSHIKAMANO KUPITIA FUTARI NA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeandaa hafla maalumu ya futari kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum k
MNEC JUMAA ASEMA MIAKA MINNE YA RAIS DKT SAMIA IMEKUWA YA MAFANIKIO MAKUBWA , ATAJA MAMBO MAKUBWA MANNE MUHIMU Na Gustaphu Haule, Pwani.MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kupitia Jumuiya ya Waza
EmoticonEmoticon