Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Victor Swella akitoa elimu ya juu ya umuhimu wa maadili kwa watumishi wa Afya mapema leo iliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo
Na Oscar Assenga, BOMBO
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Mkoa wa Tanga imekutana watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bombo na kuwapa elimu juu ya umuhimu wa maadili kwa watumishi wa Afya.
Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Victor Swella alisema kwamba watumishi katika kada ya afya wana wajibu mkubwa kuhakikisha wanafuata viapo vyao vya maadili wakati wanapotoa huduma kwa wananchi.
Swilla alisema kwamba lazima watumishi wahakikisha wanatekeleza majukumu yao vema kwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi ambao wanawahudumia .
“Tunashukuru leo tumekuja kukumbushana juu ya umuhimu wa maadili kwa watumishi wa Afya hivyo lazima mtambue kwamba mmebeba dhamana kubwa ya kutoa huduma kwa wananchi hivyo kila wakati hakikisheni mnazingatia viapo vyenu “Alisema
Hata hivyo Kamanda huyo aliwataka watumishi kuepuka kuchukua rushwa kutoka kwa wateja sambamba na kukemea suala la rushwa ngono kwa maana inaweza kuwa chanzo cha kuzorotesha utoaji wa huduma.
EmoticonEmoticon