SERIKALI YAAGIZA SEKTA ZOTE KUTUMIA WANUNUZI WENYE SIFA

December 13, 2023





Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Zanzibar, Bw. Arafat Haji, ambapo Shirika hilo ni mdhamini mkuu wa Kongamano la 14 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi linalofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa - AICC, jijini Arusha.
Waziri wa Fedha, Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiziagiza sekta zote nchini kuhakikisha zinawatumia wataalam wa Ununuzi na Ugavi wenye sifa kwenye shughuli zao, wakati wa Kongamano la 14 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi linalofanyika katika ukumbi wa AICC, jijini Arusha.







Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) akiwa ameshika tuzo ya ushiriki wa Kongamano la 14 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi linalofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa - AICC, jijini Arusha, alilokabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Jacob Kibona

Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma, Dkt. Frederick Mwakibinga, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Bw. Jacob Kibona (katikati) na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, kabla ya kuanza kwa Kongamano la 14 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi, jijini Arusha.


Wataalam wa Ununuzi na Ugavi wakiwa katika Kongamano la 14 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi, linalofanyika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa- AICC, jijini Arusha.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Bw. Jacob Kibona (wa sita kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya PSPTB na viongozi wa Mkoa wa Arusha kabla ya kuanza kwa Kongamano la 14 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi linalofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa - AICC, jijini Arusha.

HABARI

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »