MPANGO WA TAIFA WA MAENDELEO UWE NA SURA YA UTAIFA KWA VITENDO

November 08, 2023


Na Mwandishi Wetu Dodoma.

MBUNGE wa Viti Maalumu Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe Neema Lugangira ametaka Mpango wa Taifa wa Maendeleo uwe na sura ya Utaifa kwa vitendo badala ya kuyagawa maeneo nchini.

Lugangira aliyasema hayo wakati akichangia mpango huo Bungeni na alisema wanapojadili mpango wa maendeleo ya Taifa anaamini ni muhimu kwa Serikali kuhakikisha maendeleo ya Taifa yanatawanywa kwenye maeneo yote ya nchi.

Alisema kwa kufanya hivyo kutapelekea wao kuweka mipango thabiti ambayo itatafuta nyenzo na njia mbalimbali za kiunua mikoa ambayo ipo kwenye hali ya umaskini.

Mbunge Lugangira alisema ili mikoa hiyo nayo iweze kuendelea kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi na kuchangia pato la Taifa jambo ambalo Rais Dkt Samia Suluhu amekuwa akilisema mara nyingi hata katika ziara yake alipokwenda mkoani Kagera alisema kwa Jiographia na mambo yake haupaswi kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa umaskini nchini.

Alielekeza ifanyike tathimini mbalimbali na kuona namna ya kuihusisha kwenye Serikali ili mkoa huo na pamoja na mikoa mengine yenye kufanana na hiyo iweze kuinuka kiuchumi.

“Mh Mwenyekiti katika hotuba ya mpango wa maendeleo ya Taifa haijaeleza wazi namna gani Serikali imejipanga kuweka mikakati dhabiti ya kuinua mikoa yenye hali ya umaskini na haijaweka mipango mahususi wa kuona namna gani ya kutawanya maendeleo ya nchi yetu”Alisema

Alieleza kwamba kwa harakarahaka anajielekeza kwa Mkoa wa Kagera ambao unapakana na nchi tatu za Afrika Mashariki Uganda, Rwanda na Burundi ikiwemo uwepo wa asilimia kubwa zaidi ya ziwa Victoria pia wana Ranchi Tano na una ardhi yenye rutuba pamoja na misimu miwili ya mvua lakini bado inashangaza kuona mkoa unaongoza kwa umaskini.

“Hivyo kama nchini tunaweza kujiuliza kwanini ipo hivyo jambo la kwanza wameshindwa kuona nambna wanaweza kutumia maeneo ya kimkakati ili yaweza kufungua uchumi wa Taifa letu”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba Mkoa wa Kagera unaweza kuwa kitovu cha Taifa cha kuunganisha Biashara kwa nchi za Ukanda wa nchi Afrika Mashariki (Rwanda, Burundi na Uganda) na ili kufanya hivyo lazima uwepo wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa.

Aidha, Lugangira alimpongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuunda wizara mahususi ya Ofisi Rais inayosimamia mipango na uwekezaji na kuunda tume ya mipango.

Pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo Profesa Kitila Mkumbo na pamoja na Lawarance Mafuru naye kwa kuteuliwa wote kuongoza wizara hiyo kwani ni majembe na wanatosha

Alisema jambo ambalo hawana na hawaelewi hilo litatekeleza vipi,hawana soko kuu la biashara za mazao ya mifugo,kilimo na uvuvi na tatu hakuna mkakati dhabiti wa kuona zile Ranchi tano zinaweza kuwekewa mikakati ili kuchangia maendeleo,hawana viwanda vya kutosha vya samaki

Mbunge huyo alisema pia fedha za misaada pamoja na miradi ya maendeleo kutoka kwa wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa hayatawanywi ipasavyo kwenye nchi yetu unakuta ni maeneo machache hayo hayo wadau wanakwenda halihali Serikali inapaswa kuweka jitihada za makusudi kuhakikisha inatawanywa kwenye nchi yetu.

Alisema kwamba suala lingine ni kuwa mkoa wa Kagera ni ya sita kwa wingi wa watu bado Hospitali ya Mkoa wa Kagera ni sawa sawa na ya wilaya hadi kufikia kwamba hivi karibuni hadi miezi 18 iliyopita ndio walipata vifaa tiba kwa ajili ya watoto njiti kupitia jitihada zake kwa kushikrikiana na Shirika la Doris Molel Foundation.

“Leo hii watoto 780 wameweza kuokolewa maisha yao na hii inaonyesha mkoa huu kwenye sekta ya afya bado wako nyuma na mkoa huo ndio mara nyingi unapata kadhia nyingi kunapotokea milipuko ya magoinjwa hapa nchini lakini bado uwekezaji wa sekta ya afya kwenye mkoa huo haujaridhisha”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba mkoa huo hawana hata chuo kikuu kwenye mkoa huo ambacho kingweza kupata wanafunzo kutoka nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda, Burundi, Rwanda,

“Mh Mwenyekiti jambo lingine ni kwamba Serikali ilipoandaa Sagoti ya Tanzania ilikuwa na lengo la kuona namna gani ya uwekezaji utakapofanyika ili kuweza kuimarisha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kwenye mikoa ya nyanda za juu kusini ili miaka kadhaa Taasisi kama hiyo iweze kuanzishwa kwenye mikoa mengine ya kanda nyengine hivyo jambo hilo linachangia kupelekea maendeleo kwenye sehemu moja ya nchi na amikoa mengine kuendelea kubaki kuewa nyuma”Alisema

Mbunge Lugangira alisema Mkoa wa Kagera hadi leo ndio unaongoza kwa idadi ya watoto wenye utapiamlo lakini hawana mradi wowote wenye kupambana na hali hiyo lakini wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuwapelekea Mkuu wa mkoa Fatuma Mwasa na Katibu Tawala wa Mkoa huo (RAS) Toba Nguvila ambao wamekuwa na maono makubwa ya kuendelea mkoa huo kutoka uliopo ili uweze kuchangia pato la mkoa huo.

Mbunge huyo alisema kwamba alimuona Waziri Profesa Kitila Mkumbo atakapohitimisha hoja hiyo awaeleza bayana kwamba mpango wa maendeleo ya Taifa unakuwa wa vitendo kwa nchi ya Tanzania bila kuacha maeneo mengine nyuma kama vile Mkoa wa Kagera na Mengineyo kwa kufanya hivyo wanaweza kusema sasa wana mpango wa maendeleo ya Taifa


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »