Na
Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule ametoa rai kwa watumishi hasa wa
mkoani Dodoma kuiga mfano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF) wa kuhamasisha watumishi wake kupanda miti katika maeneo mbalimbali ili
kuendelea kutunza mazingira.
Mhe.
Senyamule ameyasema hayo leo mkoani Dodoma wakati akifunga semina ya wastaafu
watarajiwa wa Mfuko huo iliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Septemba 25 - 26,
2023 mkoani humo.
Mhe.
Senyamule ameipongeza PSSSF kwa kuunga
mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambapo
mpaka sasa PSSSF imegawa miche ya miti kwa wastaafu watarajiwa na waliostaafu
sasa wanafikia 739,000,
"Nimefurahi
kusikia kuwa mmewashirikisha watumishi wa PSSSF kwa kuhakikisha kila mtumishi
anapanda na kuitunza miche kumi ya miti, kampeni ambayo mmepanga iendelee hadi
Disemba 2023 ambako mnatarajia mtakuwa mmepanda miche takribani milioni 7. Mimi
na wenzangu mkoani, tunalipokea jambo hili jema kwa mikono miwili na natoa rai
kwa watumishi wengine kuiga mfano huu". Amesema Mhe. Senyamule.
Awali
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bi. Beatrice Musa – Lupi amesema kuwa Mfuko huo
unatambua na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na mabadiliko
ya tabianchi ambapo umetoa mche mmoja wa mti kwa kila mstaafu mtarajiwa wa
PSSSF aliyehudhuria semina wanazozitoa
lengo likiwa ni kila mmoja aweze kuupanda na kuutunza mche aliopatiwa.
"Pia
kwa kushirikiana na watumishi wa PSSSF tutaendesha kampeni ya kuhakikisha kila
mtumishi anapanda na kuitunza miche kumi ya miti, kampeni hii itaendelea hadi
Disemba 2023 ambapo tunatarajia kuwa tumepanda miche takribani milioni moja
katika maeneo mbalimbali", amesema bi. Beatrice.
Kwa
upande wake Mstaafu mtarajiwa, Mhandisi Salum Omary ameishukuru PSSSF kwa
kugawa miti kwa wastaafu watarajiwa ili nao waendelee kuunga mkono juhudi za
Serikali katika kutunza mazingira. Aidha, ametoa rai kwa wastaafu watarajiwa
wenzie kuendelea kupanda miti zaidi ya hiyo waliyopewa na PSSSF.
EmoticonEmoticon