PSSSF YATOA MICHE YA MITI KWA WANACHAMA WAKE KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

September 12, 2023

 

 NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DAR ES SALAAM

Katika kutambua na
kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi,
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetoa miche kwa
wastaafu watarajiwa wa Mfuko huo waliokuwa wakihudhuria semina elekezi ya kujiandaa
na maisha ya kusataafu utumishi wa Umma.

Semina hiyo ambayo ilifunguliwa
Septemba 11, 2023 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, imefungwa Septemba 12, 2023
na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba.



CPA.
Kashimba alisema, PSSSF inatarajia kuwa na wastaafu 11,000 katika mwaka wa
fedha wa 2023/24 na zoezi la ugawaji miche pia linafanyika kwenye mikoa mingine
ambako nako wastaafu watarajiwa wa Mfuko huo wanapatiwa semina kama hiyo.

“Mfuko
umepanga pia kugawa miche hiyo kwa wanachama wake 739,000 kote nchini.” Alisema

Akihutubia
katika kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi lililofanyika jijini Nairobi
Nchini Kenya, Septemba 6, 2023, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan, alisema kuna hatari kubwa, na hatua inapaswa
kuchukuliwa sio kesho bali leo na haswa sasa ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Tayari
Jumuiya ya Kimataifa imemtambua Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo Septemba 12,
2023 Bodi ya Ushauri ya Kituo cha Dunia cha Uhimilivu wa Mabadiliko ya
Tabianchi (Advisory Board of the Global Centre on Adaptation – GCA), imemteua kuwa
Mjumbe wa bodi hiyo.

Akieleza
zaidi kuhusu umuhimu wa kupanda miti, Mkurugenzi Mkuu huyo wa PSSSF alisema  “Upandaji miti unasaidia sana katika
kukabiliana na janga hili la mabadiliko ya Tabianchi ambayo ni hatari si kwa
mazingira peke yake bali hata viumbe vilivyopo katika mazingira haya, tukiwemo
na sisi binadamu.” Alisema CPA. Kashimba

“Pia
kwa kushirikiana na watumishi wa Mfuko tutaendesha kampeni ya kuhakikisha kila
mtumishi anapanda na kuitunza miche kumi ya miti, kampeni hii itaendelea hadi
Disemba 2023 ambako tunatarajia tutakuwa tumepanda miche takribani million 7.

“Hivyo
ili kuanza kampeni hii mahsusi, katika semina hii kila mwanasemina na wafanyakazi
watapatiwa angalau mche mmoja wa mti kwa ajili ya kupanda na kutunza”

Aidha
CPA. Kashimba aliwaasa wastaafu hao watarajiwa kuzingatia yale waliyojifunza lakini
kubwa kujiepusha na matapeli ili wastaafu hao watarajiwa waendelee kuishi maisha
mazuri.

“Genge
hili lina nguvu sana tusilipuuze, Mafao ndio turufu yetu ya mwisho tuyatunze.” Aliasa.

Akizungumzia
uamuzi huo wa PSSSF, Msaatu mtarajiwa Bw. Laurian Mganga, alimpongeza Mkurugenzi
Mkuu wa PSSSF CPA. Hosea Kashimba na uongozi mzima wa Mfuko huo kwa uamuzi wa kuwapatia
elimu ya kujiandaa kabla ya kustaafu, lakini pia kuwapatia kila mstaafu mche mmoja
wa kupanda ili kutunza mazingira.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, akiwa amebeba mche wakati wa zoezi la ugawaji miche kwa wastaafu watarajiwa pamoja na watumishi wa Mfuko huo.

 

Watumishi wa PSSSF wakiwa wamebeba miche ya miti tayari kwa zoezi la kuigawa kwa washiriki

Mtumishi wa PSSSF, Bi. Nelu Mwalugaja (kushoto), akigawa miche kwa wastaafu watarajiwa

 

Baadhi ya wastaafu wakiangalia miche waliyopewa

CPA. Kashimba, akizungumza na wastaafu watarajiwa wakati wa kufunga semina hiyo Septemba 12, 2023

CPA. Kashimba, akiagana na mmoja wa wastaafu watarajiwa mwishoni mwa semina hiyo.

CPA. Kashimba akiongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa baada ya kufunga semina hiyo.

 

Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa, akizungumza na wastaafu watarajiwa wa mkoa wa Dar es Salaam, Septemba 12, 2023.

 

 

Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, PSSSF, Bw. James Mlowe, akizungumza na wastaafu watarajiwa wa mkoa wa Dar es Salaam, Septemba 12, 2023.
Mkurugenzi wa Fedha PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi (kushoto), akiteta jambo na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Bw. James Mlowe.

 

 

Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa, akizungumza na washtaafu watarajiwa wa mkoa wa Dar es Salaam, Septemba 12, 2023.

 

 

 

 

 

Meneja wa PSSSF, Kanda ya Ilala, Bi. Uphoo Swai

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »