Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
WIZARA YA
MALIASILI NA UTALII
Simu Na: +255 026 2321566
Nukushi: +255 026 2321514
Barua pepe: ps@mnrt.go.tz
|
|
Mtaa wa
Kilimani,
Barabara
ya Askari,
S.L. P 1351,
40472-DODOMA
|
MKUU WA KANDA
- PORI LA AKIBA RUKWA ASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (Mb) amemsimamisha kazi
Bwana Emmanuel Barabara, Mhifadhi Wanyamapori Mkuu ambaye pia ni Mkuu wa Kanda
– Pori la Akiba Rukwa, lililopo wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi, kuanzia jana
tarehe 10 Machi, 2018 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Dk.
Kigwangalla amechukua uamuzi huo kufuatia taarifa za raia wema kuwa Bwana
Barabara amekuwa akishirikiana na majangili katika kuhujumu rasilimali za
misitu nchini.
Aidha,
Waziri Kigwangalla ameagiza iundwe Kamati ya Uchunguzi ili kubaini ukweli wa
tuhuma hizo, na endapo mtuhumiwa huyo atakutwa na hatia, hatua kali za
kinidhamu ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma
ili iwe fundisho kwa wengine.
Tunatoa
onyo kali kwa watumishi wa Wizara wanaojihusisha na vitendo vya uhujumu wa
rasilimali za Misitu, Wanyamapori na Malikale kuacha mara moja kwani hatutosita
kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na
vitendo hivyo ikiwemo kufukuzwa kazi.
Watumishi
wote wa Wizara wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo
mbalimbali iliyowekwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ya
uhifadhi wa rasilimali za nchi kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Dr. Aloyce K. Nzuki
KAIMU KATIBU
MKUU
11 Machi, 2018