UHAMIAJI TANGA YAWAKUMBUSHA VIONGOZI WA VIJIJI NA KATA KUHUSU WAHAMIAJI HARAMU WANAOKAMATWA KWENYE MAENEO YAO

February 16, 2018
VIONGOZI wa Vijiji na Kata wilayani Mkinga wametakiwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji Mkoani Tanga kwa kutoa taarifa ya juu ya uwepo wa wahamiaji haramu kwenye maeneo yao ili kuweza kuzibiti na kukomesha vitendo vya namna hiyo.
Hayo yalibanishwa hivi karibuni na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga,Crispin Ngonyani wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na kukamatwa kwa wahamiaji haramu 16 katika kijiji cha Mzava Kata ya Duga wilayani Mkinga.

Licha ya kukamatwa kwa wahamiaji hao lakini walikamatwa watanzania wanne ambao wanasaidia kuwasafirisha kutoka sehemu moja hadi nyengine wanapoingia wilayani Mkinga.

Alisema lazima viongozi hao wakishirikiana na wananchi wao kuwafichua wahamiaji hao wanapoonekana kwenye maeneo yao ili kuweza kuzibiti vitendo vya uingiaji wake kwenye maeneo mbalimbali.

Aidha alisema wahamiaji hao wamekuwa wakikamatwa mara nyingi wilayani humo kutokana na kupakana na nchi jirani ya Kenya hivyo wanapofika nchini Kenya wanaingia Horohoro kutumia kama njia ya kuelekea nchini Afrika Kusini.

“Kwani ukiangalia wahamiaji wengi wamekuwa wakikamatwa wilayani Mkinga kwa sababu upande wa mashariki wanaingia nchini Ethiopia ambapo wanapita Mombasa nchini Kenya na baadae Horohoro halafu wanakwenda kusini mwa Tanzania “Alisema.

Alisema wahamiaji hao wamekuwa wakipitia njia za mapori kutoka nchini mwao hadi kufika wilayani mkinga na baadae kuendelea na safari zao kwa kupitia njia hizo mpaka wanapokwenda.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »