Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiteta jambo
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira,
January Makamba wakati wa mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la
Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mkutano
huo ulilenga kujadili na kusaini makubaliano mbalimbali ya namna bora
ya kusimamia sekta hizo katika nchi wanachama.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba
(kulia) akisaini baadhi ya makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa
tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi
za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa
EAC jijini Arusha. Mkutano huo ulilenga kujadili na kusaini makubaliano
mbalimbali ya namna bora ya kusimamia sekta hizo katika nchi wanachama.
Wanaoshuhudia ni Mawaziri wa Mazingira kutoka Uganda na Kenya.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (wa pili
kulia) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Bi. Katerina Rangnitt
wakiangalia baadhi ya michoro ya katuni za kuhamasisha uhifadhi wa
mazingira muda mfupi baada mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la
Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mradi
huo ya katuni unafadhiliwa na Serikali ya Sweden kwa ushirikiano na
Serikali ya Tanzania.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba
wakimsikiliza mmoja ya wachora katuni za kuhamasisha uhifadhi wa
mazingira muda mfupi baada mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la
Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mkutano
huo ulilenga kujadili na kusaini makubaliano mbalimbali ya namna bora
ya kusimamia sekta hizo katika nchi wanachama.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
(PICHA ZOTE NA HAMZA TEMBA-WMU)