Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi mbalimbali
pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika sherehe ya
kukaribisha Mwaka mpya kwa Mabalozi hao wanaowakilisha nchi zao hapa
nchini(Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje Balozi
Dkt. Augustine Mahiga katika picha ya pamoja na Mabalozi mbalimbali
wanaowakilisha nchi zao hapa nchini katika Hafla ya kukaribisha Mwaka
mpya 2018 kwa mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kuwakaribisha Mabalozi
mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa hafla ya
kukaribisha mwaka mpya kwa Mabalozi hao.
Baadhi ya Mabalozi hao
wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika
Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU