Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro (wapili kushoto), akikagua baadhi ya vielelezo katika kituo Kikuu
cha Polisi wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati akiwa katika ziara ya
kikazi ya kuzungumza na maofisa na askari mkoani humo, IGP Sirro
amewataka askari kufanyakazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya kazi
pamoja na kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia. Picha na Jeshi la
Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro, akipokea salamu ya heshima kutoka kwa askari wa kikosi maalum
cha Jeshi hilo wakati alipowasili Bariadi mkoani Simiyu kwa ziara ya
kikazi IGP Sirro pia aliwataka askari kutojihusisha na vitendo vya
rushwa na kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi wanaowahudumia. Picha
na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro, akiweka saini kwenye kitabu cha wageni wakati alipowasili katika
Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuzungumza na wajumbe wa
kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo (hawapo pichani), kulia ni Mkuu
wa mkoa huo Mhe. Antony Mtaka. Picha na Jeshi la Polisi.