Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.
Adolf Mkenda akifafanua jambo kwa washiriki wa kikao cha kujadili
maandalizi ya wiki ya Tanzania nchini Kenya mapema hii leo jijini Dar es
Salaam. Kuia ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dk. Pindi Chana na
katikati ni Mtendaji Mkuu wa TANTRADE Edwin Rutageruka.
Baadhi
ya washiriki wa kikao cha kujadili maandalizi ya wiki ya Tanzania
nchini Kenya wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani)
wakati wa kikao hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Eliphace Marwa - MAELEZO
Jonas Kamaleki- MAELEZO.
Serikali
imetoa wito kwa wafanyabiashara wa Tanzania kupeleka bidhaa zao katika
soko la Kenya ili kupanua wigo wa masoko ya bidhaa zao.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda wakati wa
kikao cha Maandalizi ya Wiki ya Tanzania nchini Kenya.
Prof.
Mkenda alisema kuwa ni nia ya Serikali kuhakikisha watanzania wanapenya
katika masoko ya kimataifa ili kuongeza pato la mtu binafsi na la Taifa
kwa ujumla.“Hali
ya biashara kwa sasa ni nzuri sana, hivyo vikwazo visiwepo kabisa kati
ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki”, alsiema Prof.
Mwaikenda.
Kwa
upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Balozi, Dkt. Pindi Chana
amesema kuwa watanzania inabidi wathubutu na kuingia katika soko la
Afrika Mashariki hususan soko la Kenya.Amesema
kuwa wafanyabiashara wa Kitanzania wasiogope kuingia katika masoko ya
nje ya nchi, wajitahidi ili waweze kuongeza vipato kutokana na ukubwa wa
soko lililopo nchini na Kenya kwa ujumla.
“Mkifanya
biashara Kenya mtaongeza mitaji, ajira na kipato kwa ujumla kwani nchi
hizi mbili zina zaidi ya watu milioni 90”, na hii inaendana na falsafa
ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli ya Uchumi wa Viwanda, hivyo hatuna budi
kufuata maono ya Kiongozi wetu na kutengeneza na kuuza bidhaa za
viwandani nje ya nchi”, alisema Balozi Pindi Chana.
Akizungumza
katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Juma Ali Juma amesema wazo la kufungua
soko la Kenya ni zuri na kumpongeza Balozi Pindi Chana kwa ubunifu huo.
Aliongeza
kuwa anafahamu kuwa zipo changamoto ndogo ndogo katika masoko lakini
zinafanyiwa kazi ili kuhakikisha biashara kati ya Tanzania na Kenya
inaenda vizuri.Bwana
Juma alisisitza kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini inabidi ziwe na ubora
na kuwa na vifungashio bora ili kumvutia mteja kununua.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (TANTRADE),
Edwin Rutageruka amesema watanzania waende Kenya wakijiamini kwani
bidhaa zao zinahitajika sana.Aliwataka wafanyabiashara kujenga maghala mipakani ili kutunza bidhaa zao humo na kuziuza kwa bei nzuri wakati muafaka.
Akichangia
mada katika kikao cha maandalizi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye aliwaomba seka binafsi
wajitokeze ili kupeleka bidhaa zao nchini Kenya na kuitumia hiyo fursa
katika kukuza biashara zao.
Simbeye
aliiomba Serikali kuwapeleka waambata wa kibiashara kwenye balozi za
Tanzania Duniani ili washughulikie suala la masoko na fursa nyingine za
kibiashara.Kikao
hiki cha maandalizi kimetokana na maono ya Mhe. Balozi, Dkt. Pindi
Chana ambaye amebuni wazo la kufanya wiki ya Tanzania nchini Kenya kwa
ajili ya kutafuta soko la bidhaa za Tanzania ambayo itafanyika 26
Aprili, 2018 na itadumu kwa wiki moja.