Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary
Mwanjelwa akiwasihi waumini kumuunga mkono na kumuombea Rais Magufuli wakati
akitoa salamu kwenye ibada ya Siku ya Wazee iliyofanyika katika kanisa La
Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) lililopo
Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini Mbeya, Leo 1 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary
Mwanjelwa akimlisha chakula mmoja ya wazee waliohudhuria ibada ya Siku ya Wazee
iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing
Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini
Mbeya, Leo 1 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary
Mwanjelwa pamoja na Viongozi wengine wakiongoza maombi wakati wa ibada ya Siku
ya Wazee iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus
Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga
Jijini Mbeya, Leo 1 Januari 2018.
Miongoni mwa wazee waliohudhuria ibada ya Siku
ya Wazee iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus
Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga
Jijini Mbeya, Leo 1 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary
Mwanjelwa akifanyiwa maombi na viongozi wa dini wakati wa ibada ya Siku ya
Wazee iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus
Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga
Jijini Mbeya, Leo 1 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary
Mwanjelwa akishiriki chakula cha mchana na wazee waliohudhuria ibada ya Siku ya
Wazee iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus
Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga
Jijini Mbeya, Leo 1 Januari 2018.
Na Mathias Canal,
Mbeya
Wananchi Mkoani Mbeya wametakiwa kuunga mkono kwa vitendo juhudi
za uwajibikaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.
Mwito huo umetolewa Leo 1 Januari 2018 na Naibu Waziri wa Wizara
ya Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa wakati akitoa salamu kwenye ibada ya Siku ya
Wazee iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus
Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga
Jijini Mbeya.
Alisema kuwa Rais Magufuli na serikali anayoingoza anawathamini
kwa kiasi kikubwa wazee kote nchini kwani kwa umri wao ni sehemu ya turufu
muhimu kimawazo na busara katika utendaji ndio maana Mke wake Mhe Mama Janeth
Magufuli hushirikiana na wazee waliopo katika makundi mbalimbali katika huduma
za kijamii.
Alisema kuwa serikali hii ya awamu ya Tano inayochagizwa na
kauli mbiu isemayo "HAPA KAZI TU" inawakumbusha na kuwahamasisha
wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuinua haraka uchumi wa mtu mmoja mmoja na
Taifa kwa ujumla.
Katika ibada Hiyo Mhe Mwanjelwa ameshiriki chakula cha mchana na
wazee waliohudhuria ibada Hiyo ya siku ya wazee kutoka Kata ya Manga na Sinde
ikiwa ni ishara ya mapokezi mema ya Mwaka Mpya 2018.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo aliongoza
waumini wa kanisa la Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre
T. Ministry) kumuombea Rais Magufuli sambamba na serikali kwa ujumla ili
wananchi waendelea kujivunia matunda ya Rais Magufuli ambaye Duniani kote
anasifika kwa umakini na ushupavu.
Alisema kuwa zoezi hilo linapaswa kuwa endelevu kwa kanisa hilo
kushirikiana kwa Karibu na wazee huku akisema kuwa litakuwa jambo zuri na
muhimu zaidi endapo litafanyika kwa ajili ya wazee wa Mkoa mzima wa Mbeya.
"Wazee ni Tunu, kuwa Mzee ni Baraka kwani hata vijana ni
wazee wajao, Lakini niwasihi kuendelea kuwatumia wazee kwa ushauri wa kijamii
pia kidini lakini zaidi Mwaka Mpya 2018 uwe Mwaka wa Mafanikio kwetu
sote:" Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Mhe Mwanjelwa Alisifu uongozi wa kanisa hilo kwa kumualika
kushiriki nao katika ibada hiyo huku akiwapongeza kwa kufanya ibada ya kiroho
lakini pia ibada ya kimwili kwa ushirikishaji wa jamii.
Naye Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Huduma ya Maombezi na
Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) Mchungaji Capson Masimbani
alimpongeza Mhe Mwanjelwa na kusema kuwa ni kiongozi mwenye kujali wananchi
pasina kubagua itikadi za dini zao.
Alisema kuwa ni Viongozi wachache nchini ambao wana unyenyekevu
kama yeye huku akimsihi kuendelea na busara na hekima Hiyo.
Sambamba na hayo Mhe Naibu Waziri wa Kilimo aliunga mkono juhudi za kanisa hilo kwa kuandaa sherehe hiyo ya siku ya wazee kwa kuwapatia mifuko 66 ya sukari wazee hao.