AZAM, YANGA KUPIGWA SAA 10
CHAMAZI
Mchezo
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018 kati ya Azam FC na
Young Africans utachezwa saa 10 jioni Azam Complex Chamazi.
Mchezo
huo namba 115 utachezwa Jumamosi Januari 27, 2018.
Viingilio
kwenye mchezo huo ni shilingi elfu kumi(10,000) kwa Jukwaa Kuu na shilingi elfu
saba (7,000) kwa majukwaa ya kawaida.
Waamuzi
wa mchezo huo wote ni kutoka Dar es Salaam ambapo muamuzi wa kati ni Israel
Nkongo akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Josephat Bulali na mwamuzi
msaidizi namba mbili Soud Lila, mwamuzi wa akiba Elly Sasii wakati Kamishna wa
mchezo huo ni Omar Abdulkadir.
MCHEZO WA MWADUI VS NJOMBE MJI
WASOGEZWA
Mchezo
namba 114 kati ya Mwadui FC ya Shinyanga na Njombe Mji ya Njombe uliokuwa
ufanyike Ijumaa Januari 26, 2018 imesogezwa kwa siku moja kupisha mazishi ya
aliyekuwa kocha msaidizi wa Mwadui Jumanne Ntambi.
Mchezo
huo sasa utachezwa Jumamosi, Januari 27, 2018.
Kocha
huyo msaidizi wa Mwadui alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu
kabla ya kufikwa na mauti.
CAF
YATAJA WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA MECHI YA YANGA NA SAINT LOUIS FC LIGI YA
MABINGWA
Shirikisho la Mpira wa miguu Barani Africa CAF limetaja
waamuzi watakaochezesha mchezo wa kwanza na mchezo wa pili wa Ligi ya mabingwa
Africa kati ya Yanga ya Tanzania dhidi ya Saint Louis FC ya Seychelles.
Mchezo wa kwanza utachezwa Februari 10, 2018 uwanja wa
Taifa na utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia na Kamishna wa mchezo akitokea
nchini Namibia.
Mwamuzi wa kati atakuwa Belay Tadesse Asserese akisaidiwa
na mwamuzi msaidizi namba moja Tigle Gizaw Belachew na mwamuzi msaidizi namba
mbili Kinfe Yilma Kinfe wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Amanuel Heleselass
Worku na Kamishna Frans Vatileni Mbidi.
Mechi ya pili itakayochezwa Seychelles kati ya Februari 20
na 21,2018 itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar na kamishna atatoka
Mauritius.
Mwamuzi wa kati atakuwa Andofetra Avombitana Rakotojaona
akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Lionel Hasinjarasoa Andrianantenaina
na mwamuzi msaidizi namba mbili Pierre Jean Eric Andrivoavonjy na mwamuzi wa
akiba Hamada el Moussa Nampiandraza,kamishna wa mchezo huo Ahmad Nazeer Hossen
Bowud.
WAAMUZI WA SUDAN KUSINI KUCHEZESHA SIMBA VS GENDARMERIE
TNALE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRICA
Waamuzi kutoka Sudan Kusini wameteuliwa na Shirikisho la
Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati
ya Simba ya Tanzania na Gendarmerie Tnale ya Djobouti itakayochezwa Februari 21,2018
Uwanja wa Taifa.
Mwamuzi wa kati atakuwa Alier Michael James akisaidiwa na
mwamuzi msaidizi namba moja Abdallah Suleiman Gassim ,mwamuzi msaidizi namba
mbili Gasim Madir Dehiya wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Kalisto Gumesi Simon
Samson na Kamishna wa mchezo huo kutoka Botswana ni Mmonwagotlhe Edwin Senai.
Mchezo wa marudiano utakaochezwa Djibouti kati ya Februari
20 na 21,2018 wenyewe utachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi na Kamishna wa
mchezo atatokea nchini Rwanda.
Mwamuzi wa kati ni Eric Manirakiza akisaidiwa na mwamuzi
msaidizi namba moja Pascal Ndimunzigo,mwamuzi msaidizi namba mbili Willy
Habimana,mwamuzi wa akiba Pacifique Ndabihawenimana na kamishna Gaspard
Kayijuka.
WATANZANIA
TISA KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA LIGI YAMABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRICA
Waamuzi nane kutoka
Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF
kuchezesha mechi za Ligi ya Mabingwa Africa na Kombe la Shirikisho.
Waamuzi wanne wameteuliwa kuchezesha mchezo wa Ligi ya mabingwa
kati ya Lydia Ludic Burundi Academic ya Burundi na Rayon Sports ya Rwanda.
Mwamuzi Mfaume Ali Nassoro atakuwa mwamuzi wa kati
akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Frank John Komba wakati mwamuzi
msaidizi namba mbili atakuwa Soud Idd Lila na mwamuzi wa akiba Israel Omusingi
Njunwa Mujuni huku kamishna wa mechi hiyo akitokea nchini Zimbabwe Gladmore
Muzambi.
Mchezo huo utachezwa kati ya Februari 20 na 21, 2018
nchini Burundi.
Waamuzi wengine wanne wa Tanzania watachezesha mchezo wa
Kombe la Shirikisho kati ya Masters Security Services FC ya Malawi dhidi ya
Atletico Petroleos de Luanda ya Angola nutakaochezwa kati ya Febriari 20 na
21,2018 nchini Malawi.
Elly
Ally Sasii atakuwa mwamuzi wa katikati kwenye mchezo huo akisaidiwa na Mwamuzi
msaidizi namba moja Salim Mkono Mohamed na mwamuzi msaidizi namba mbili
Ferdinand Chacha na mwamuzi wa akiba Alphonce Mwandembwa Emmanuel wakati
kamishna wa mchezo huo atatokea Ethiopia Luleseged Gegashaw Asfaw.
Wakati huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa
CAF limemteua Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Ndugu
Michael Richard Wambura kuwa Kamishna wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani
Africa kati ya Bidvest Wits ya Africa Kusini na Pamplemousses SC ya Mauritius
utakaochezwa Februari 10, 2018 kwenye uwanja wa Johannesburg-Bidvest.
Wambura atasimamia mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi
kutokea Seychelles.
Mwamuzi wa kati Nelson Emile Fred akisaidiwa na Hensley
Danny Petrousse na James Fedrick Emile wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Allister
Barra
Huu unakuwa ni muendelezo kwa CAF kuteua viongozi
mbalimbali wa Tanzania kuwa makamishna wa mechi zinazoandaliwa na Shirikisho
hilo.
Tayari Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia licha ya kuteuliwa
kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya fainali za Africa kwa
wachezaji wanaocheza ndani CHAN pia ameteuliwa mara mbili kuwa Kamishna wa
mechi ya ufunguzi ya CHAN wenyeji Morocco walipocheza dhidi ya Mauritania
Februari 13, 2018 na mchezo mwingine uliowakutanisha Namibia na Zambia
uliochezwa Februari 22, 2018
Aidha mjumbe mwingine wa kamati ya utendaji Ahmed Iddi
Mgoyi naye ameteuliwa na CAF kuwa kamishna wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati
ya AFC Leopards ya Kenya dhidi ya Fosa Juniors ya Madagascar mchezo
utakaochezwa kati ya Februari 9,10 na 11,2018 nchini Kenya.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF