Kamishna wa Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela akizungumza na
waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati
alipowawataka Viongozi wote wa umma nchini kuorodhesha mali zao kisha
kukabidhi kwa Sekretarieti kabla ya Desemba 31 mwaka huu Kulia ni Afisa
Sheria Mkuu wa Sekretarieti hiyo Bw. Filotheus Manula.
Kamishna wa Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela katikati
akikaribishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Bw.
Rodney Thadeus ili kuzungumza na waandishi wa habari, wa pili kutoka
kulia ni Aisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Bw. Filotheus Manula na kushoto ni Ofisa wa Sekretarieti hiyo Bw.
Waziri Kipacha
………………………………………………………………………….
Kamishna wa Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela amewahimiza viongozi wote wa umma nchini kuorodhesha mali zao kisha kukabidhi kwa
Sekretarieti kabla ya Desemba 31 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa
habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo amesema kufanya
hivyo ni utaratibu ambao upo kwa mujibu wa sheria ,hivyo lazima
watekeleze kwa wakati na watakaoshindwa hatua za kinidhamu
zitachukuliwa dhidi yao.
, Jaji Mstaafu Nsekela ameongeza
kwamba mwisho kwa viongozi wa umma kukabidhi tamko la mali zao na
kufafanua kuwa viongozi wanaotakiwa kuorodhesha mali zao na kisha
kukabidhi Sekretarieti ya Maadili ni wale wa kuteuliwa na kuchaguliwa.
“Kila kiongozi wa umma ajaze
tamko hilo kwa kuorodhesha mali zake, mwenza wake na watoto wake walio
na umri chini ya miaka 18,”amesema.
Ameongeza kuwa viongozi ambao
wanastaafu wakati wanaingia waliorodhesha mali zao, hivyo wanapostaafu
ni lazima waoredheshe ili ifahamike wanatoka wakiwa na mali kiasi gani.
Ili kufikia malengo ya tamko
hilo kisheria linalowahusisha pia viongozi waliostaafu na wale
wanaoelekea kustaafu, Ameongeza kwamba Fomu za tamko zipo kwenye tovuti
ya sekretarieti ya maadili.
Amesema anaamini viongozi
wanafahamu wajibu wao,hivyo wafanye haraka iwezekanavyo na hasa kwa
kuzingatia muda uliobakia ni mchache.
Kuhusu viongozi wanaostaafu ambao
wamejaza tamko hilo amesema nao bado lakini katika eneo hilo kuna
changamoto yake kidogo kwani viongozi wanapostaafu inakuwa ngumu
kuwapata lakini nao watambue wanatakiwa kujaza tamko kwa mujibu wa
sheria.
Kwa upande wake, Ofisa Sheria
Mkuu wa Sekretarieti ya maadili Bw. Filotheus Manula ameongeza kuwa
ujazaji wa tamko la mali kwa viongozi wa umma ni takwa la kikatiba na
kuna adhabu kwa wasiofuata.
Ametaja adhabu hizo ni kuonywa, kushushwa cheo, kusimamishwa kazi na wakati mwingine kufukuzwa kazi.