NAIBU WAZIRI AWESO:HATUTASITA KUWACHUKULIA HATUA WAKANDARASI WAZEMBE

December 30, 2017


 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akisaini cha wageni kata ya Songea alipokuwa na mkutano wa hadhara na wananchi wakati wa ziara yake
  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akimwaga mchanga kwa ajili ya mradi huo
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua mradi huo wa maji
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimuagiza Mkandarasi wa Maji mbele ya Wananchi wa Tunduma kuhakikisha mradi wa maji unakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma za maji .
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema hatasita kumchukulia hatua mkandarasi yoyote ambaye atashindwa kukamilisha kwa wakati miradi ya maji waliopewa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kuwasimamisha.
Lakini pia ametoa wito pia wakandarasi wa magengeni kuacha kutumiwa kwenye maeneo mbalimbali kwani wamekuwa ndio chanzo cha kupelekea miradi mingi kushindwa kukamilika kwa wakati hali inayosababisha adha kubwa kwa wananchi.
Aliyasema hayo baada ya kukagua mradi wa maji wa eneo Songea katika mji mdogo wa Tundyma wilaya ya Momba mkoani Songwe ambao unatekelezwa na Mkandarasi wa Kampuni ya Best One Company ambapo aliwataka kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa waledi mkubwa ili uweze kuwa chachu ya mafanikio kwa wananchi hao.
Katika mradi huo Serikali imetolea fedha bilioni moja kwa ajili ya mradi huo ambapo Naibu Waziri huyo alizitaka zitumike kwa uangalifu mkubwa ili kuweza kuukamilisha kwa lengo la kuondoa kero kwa wananchi .
Hata hivyo alisema iwapo mradi huo utashindwa kukamilika kwa wakati hawasita kumchukulia hatua ikiwamo kumsimamisha kazi kwani hawako tayari kuona uzembe unafanyika wakati wananchi wana uhitaji mkubwa wa huduma hiyo.
“Labda niwaambie kwamba sisi kama serikali nia yetu kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi kwenye maeneo yao lakini niwaambie kuwa pia hatutamvumilia Mkandarasi yoyote ambaye akishindwa kukamilisha mradi huo kwa wakati hasa huyo ambaye anatekeleza eneo hili “Alisema Naibu Waziri Aweso.
Naye kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Momba,Juma Irando ameitaka idara ya maji wilayani humo kutowapa tenda wakandarasi wanaotuhumiwa kukwamisha juhudi za serikali za kukabiliana na tatizo la maji kuhakikisha linakwisha
Hata hivyo alisema inadaiwa kuwa baadhi ya miradi ya maji wilayani humo inashindwa kukamilika kwa wakati kutokana na uwezo mdogo kitaalamu walionao baadhi ya wakandarasi ambao wanakabidhi miradi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »