MKOA
wa Kilimanjaro, umepongezwa kwa kuitikia agizo la Rais John Magufuli la
kutaka kila mkoa ubainishe fursa za uwekezaji zilizopo na kuandaa
mwongozo wa uwekezaji.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph
Kakunda katika hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoa wa
Kilimanjaro uliondaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii
(ESRF) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Akimwakilisha
Waziri wa Nchi wa Ofisi hiyo Selemani Jafo, Naibu Waziri huyo alisema
kwamba agizo la Rais ambalo limelenga kuweka mikakati mahsusi ya
kuipeleka nchi katika uchumi wa viwanda.
Akitoa
salamu za pongezi kwa Mkuu wa mkoa, Mh. Anna Mghwira Naibu Waziri
Kakunda alisema wakati mkoa wa Kilimanjaro unatekeleza maagizo, serikali
kuu nayo inaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara ili
kuvutia wawekezaji mbalimbali.
- Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mh. Joseph Kakunda akitoa hotuba
wakati wa kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro kwa
niaba ya Waziri wa Nchi wa Ofisi hiyo, Mh. Selemani Jafo (hayupo
pichani) kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
jengo la NSSF mjini Moshi, mkoani humo.
Akizungumzia
Mwongozo huo Naibu Waziri alisema kwamba kazi ya kubaini fursa za
uwekezaji katika miradi mbalimbali yenye faida siyo tu kwa wawekezaji
pekee bali pia kwa taifa letu kupitia kodi na upatikanaji wa bidhaa na
huduma mbalimbali kwa kila eneo la nchi.
Alisema
kazi iliyofanywa na mkoa huo ina maana kubwa kwa kuwa sasa inakuwa
rahisi kwa wawekezaji wawe wa ndani au nje kujua namna ya kuwekeza
katika mkoa wa Kilimnjaro kwa kuzingatia mahitaji yao na namna
rasilimali watu na miundombinu ilivyo.
Alisema
agizo la Rais la utengenezaji wa mwongozo unakwenda sanjari na
ubainishaji na uandazi wa maeneo ya uwekezaji ili yanapotakiwa
yapatikane hima.
- Mkuu
wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira akizungumza machache kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI,
Mh. Joseph Kakunda (katikati) kutoa hotuba ya uzinduzi wa mwongozo wa
uwekezaji wa mkoa huo uliondaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP katika
hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi. Kulia
ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour.
Aliutaka
mkoa huo kuutangaza mwongozo wao kwani biashara ni matangazo katika
maeneo mbalimbali ya kimataifa na ya wawekezaji katika masoko ya hisa
kwa njia ya kielektroniki ili wavune utayari wao wa kukaribisha
uwekezaji.
Kakunda
alisema kwamba mkoa huo kwa asili unaweza kabisa kuvutia wawekezaji.
Kinachostahili kufanywa kwa sasa ni kuhakikisha kauli mbiu ya
Kilimanjaro ya Viwanda, inawezekana chukua hatua inatekelezwa kwa
vitendo.
Akizungumza
kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira
alisema kwamba Mwongozo huo utafanyiwa kazi na matunda yake yataonekana
wakati taifa linaelekea kwenye uchumi wa viwanda.
Alisema
mkoa huo una rasilimali za kutosha kuwezesha wawekezaji mbalimbali
kutekeleza adhma ya kuwa na viwanda vidogo na vya kati vinavyotumia
rasilimali kutoka mkoani.
Aliwashukuru wataalam wa ESRF waliwezesha kupatikana kwa muongozo huo na wafadhili ambao ni UNDP.
Naye
Dk Tausi Mbaga Kida, Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi
na Kijamii (ESRF) ambayo ndiyo ilipewa jukumu na Mkoa wa Kilimanjaro
kufanya utafiti na uchambuzi wa kina ili kubaini fursa za uwekezaji
zilizopo katika Mkoa, aliupongeza mkoa wa Kilimanjaro kwa kuona umuhimu
wa kuwa na mwongozo wa uwekezaji.
Aidha
katika hotuba yake hiyo alisema kuwa taasisi yake ilitengeneza sehemu
tatu za taarifa ambazo zote zililenga kutoa uwanda mpana kwa wawekezaji
kuwa na taarifa muhimu za uwekezaji katika mkoa wa Kilimanjaro.
- Mkurugenzi
Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi
Mbaga Kida akitoa taarifa kuhusu uandaaji wa Mwongozo wa Uwekezaji wa
mkoa wa Kilimanjaro ulioandaliwa na taasisi yake kwa ufadhili wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) katika hafla iliyofanyika mjini
Moshi kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF.
Alisema
katika hotuba yake kwamba ESRF ilifanikiwa kuandaa ripoti tatu ambazo
ni Ripoti ya Fursafiche katika Viwanda (Industrialization Potentials
Report), Ripoti ya Fursa za Uwekezaji (Investment Opportunities Report)
pamoja na Mwongozo wa Uwekezaji ambao Mkoa umezindua rasmi leo.
Pia
alisema kwamba Ripoti hizo zilithibitishwa na Mkoa Oktoba 12, 2017
katika warsha maalum iliyoandaliwa na Mkoa wa Kilimanjaro.
Mapema
mwaka huu Mwongozo kama huo ulizinduliwa Mkoani Simiyu ambao umeleta
matokeo makubwa ndani ya muda mfupi. Wiki mbili zilizopita mkoa wa
Mwanza nao ulizindua mwongozo wa uwekezaji. Mkoa wa Mara katika siku za
usoni unatarajiwa kuzindua mwongozo wa uwekezaji. Miongozo yote hiyo
imeandaliwa na ESRF.
Alisema
miongozo hiyo ya Uwekezaji inaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025
na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016 – 2021)
unaosisitiza ujenzi wa Tanzania ya Viwanda ili kuifikisha nchi katika
uchumi wa kati ifikapo 2025.
- Sehemu
ya wadau wa sekta binafsi, serikali, wawekezaji na taasisi mbalimbali
waliohudhuria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro
ulioandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na UNDP kwenye hafla iliyofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
Katika
hotuba yake pia Dk Kida aliiushukuru Uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro
chini ya Mkuu wa Mkoa, Anna E. Mghwira, Katibu Tawala wa Mkoa, Mhandisi
Aisha S. Amour na viongozi wengine wa mkoa na wilaya zote kwa kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa wataalamu wakati wanapita kutafuta maoni.
Aidha alitoa shukurani kwa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa ufadhili wa fedha.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa
nne kulia), Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dkt. Tausi Kida (wa tatu kushoto), Mkuu wa mkoa Kilimanjaro,
Mh. Anna Mghwira (wa nne kushoto), Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro,
Mhandisi Aisha S. Amour (wa tatu kulia) Mkuu wa Idara ya Maarifa na
Ubunifu wa ESRF Bi. Margareth Nzuki (wa pili kulia), Mtafiti Mshiriki wa
ESRF, Dkt. Hoseana Lunogelo (kulia), Watafiti vijana kutoka ESRF Bw.
Mussa Martine (kushoto) pamoja na Bw. Joseph Nyampepela Ngonyani (wa
pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakiwa wameshika nakala
za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Pia
alishukuru timu ya ESRF ikiongozwa na Bi. Margareth Nzuki, Mkuu wa
Idara ya Maarifa na Ubunifu kwa kuratibu, watafiti washiriki Prof.
Haidari Amani; Dkt. Hoseana Lunogelo na Prof. Samuel Wangwe kwa kupitia
mwongozo huu.
Aidha
aliwashukuru watafiti vijana Bw. Mussa Martine, Bw. Joseph Nyampepela
Ngonyani pamoja na Bw. John Shilinde. Aidha, alisema anatambua mchango
mkubwa aliotoa marehemu Abdallah Hassan katika uandaaji wa Mwongozo huu.
Pia
alisema ESRF ipo kwa ajili ya maendeleo ya nchi na wananchi wake na
hivyo wasisite kuwatumia pale wanapohitaji msaada wa kitaalam.
Mwongozo huu pia unapatikana katika tovuti ya ESRF na tovuti ya mkoa wa Kilimanjaro
- Mshiriki
Mtafiti wa ESRF, Dkt Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu fursa
za uwekezaji mkoani Kilimanjaro zilizoonekana wakati wa kuandaa Mwongozo
wa Uwekezaji wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mwongozo
huo ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP katika hafla fupi
iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
- Mtafiti
Mshiriki wa ESRF, Dkt. Hoseana Lunogelo (katikati) pamoja na Watafiti
vijana kutoka ESRF Bw. Mussa Martine (kulia) pamoja na Bw. Joseph
Nyampepela Ngonyani (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa
Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro ulioandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na
UNDP.
- Picha
juu na chini baadhi ya wadau na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi
wa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kilimanjaro ulioandaliwa na ESRF kwa
ufadhili wa UNDP kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
NSSF mjini Moshi, mkoani humo.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa
pili kulia) akikata utepe kuzindua rasmi Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa
wa Kilimanjaro huku Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto), Mkuu wa mkoa Kilimanjaro,
Mh. Anna Mghwira (wa pili kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour (kulia) wakishuhudia tukio hilo
katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini
Moshi.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa
pili kulia) akionyesha nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa
Kilimanjaro mara baada ya kuzindua rasmi huku Mkurugenzi Mtendaji
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida
(kushoto), Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira (wa pili kushoto)
pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour
(kulia) wakishuhudia tukio hilo katika hafla fupi iliyofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa
pili kulia) akikabidhi nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa
Kilimanjaro kwa Mkuu wa mkoa huo, Mh. Anna Mghwira (wa pili kushoto)
mara baada ya kuzindua rasmi huku Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti
za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) amoja na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour (kulia)
wakishuhudia tukio hilo katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa NSSF mjini Moshi.
- Mkurugenzi
Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi
Mbaga Kida akipeana mkono na Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi wakati wa
kukabidhi nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro
ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP kwenye hafla fupi iliyofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda na
meza kuu katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya za mkoa wa
Kilimanjaro na wadau wa maendeleo Ubalozi wa Uholanzi na taasisi zingine
huku wakiwa wameshika nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo baada
ya kuzinduliwa rasmi.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda
katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya mkoani
Kilimanjaro.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda
katika picha ya pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za serikali.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda
katika picha ya pamoja na baadhi ya wawekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda
katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa
Kilimanjaro.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda
katika picha pamoja na Sekretarieti ya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda
katika ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkuu, Rombo mkoani
Kilimanjaro.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda
katika picha ya pamoja na Bendi ya Chuo cha Polisi Moshi (CCP)
waliokuwepo ukumbini hapo kusherehesha uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji
wa mkoa wa Kilimanjaro.
- Kaimu
Mkurgenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania, Bw. Primus Kimaryo
akizungumza na kuelezea kuhusu kazi za Bodi ya Kahawa nchini mara baada
ya kuzinduliwa rasmi Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
- Kaimu
Meneja wa Kanda wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Bw Brendan Maro akitoa
salamu za TIC katika kuelekea Kilimanjaro ya Viwanda wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.
- Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda
pamoja na Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira wakiimba wimbo wa
'Tanzania Yetu' wakishirikiana na bendi ya Chuo cha Polisi Moshi (CCP)
iliyokuwa ikisherehesha uzinduzi huo.