Waziri Mpina na baadhi ya
viongozi wa wilaya ya Bukoba wakielekea katika zoezi la upigaji chapa
ng’ombe katika kata ya katerero kijijini Kyerwa leo.
Katika picha ikionekana sehemu ya ng’ombe aliyepigwa chapa katika kata ya Katerero kijijini Kyerwa leo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe
Luhaga Mpina, Mkuu wa Wialaya ya Biharamulo Bi. Saada Malunde baada ya
zoezi la kukagua uvamizi wa mifugo katika sehemu ya pori la Bugiri
Biharamuro, wengine katika picha ni askari wanyamapori wa pori hilo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe
Luhaga Mpina, Mkuu wa Wialaya ya Biharamulo Bi Saada Malunde
wakizungumza baada ya zoezi la kukagua uvamizi wa mifugo katika sehemu
ya pori la Bugiri Biharamuro.
………………………………………………………………………….
NA; MWANDISHI MAALUM – KATERERO
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Luhanga Mpina amewataka wafugaji nchini kutembea kifua mbele kwa
kumpata yeye kama Waziri mwenye dhamana ya Mifugo, Mpina ameyasema hayo
leo aliposhiriki katika zoezi la kupiga chapa Mifugo katika Kijiji cha
Kyelwa kilichopo katika kata ya Katerero halimashauri ya wilaya Bukoba
mkoani Kagera, na kuwataka viongozi kuzingatia maadili wakati wa
utekelezaji wa zoezi hilo ili kuepuka hujuma na ubaguzi kwa wafugaji.
Waziri Mpina alipofika katika
kata ya Katerero aliwakuta wafugaji wamejitokeza kwa wingi kuunga mkono
zoezi la uwekaji alama katika mifugo yao na kushiriki zoezi hilo kwa
kuonyesha msisitizo.
Mara Baada ya kushiriki zoezi
hilo, Waziri Mpina aliwataka wafugaji hao kuendelea kujitokeza kwa
wingi na kuleta mifugo yao kupigwa chapa na kusema kuwa zoezi hilo ni la
manufaa na faida kwa wafugaji kwani litaweza kuwasiadia kuhepuka
maambukizi ya magonjwa ya wanyama kwa mifugo yao kuto kuchanganyikana na
mifugo mingine sambamba na kusaidia upotevu wa mifugo.
Akiongea katika zoezi hilo diwani
wa kata ya Katerero Bw. Nuru Abdul Kabendera alisema kuwa,
amefurahishwa na ziara ya Waziri Mpina katika kata ya katerero kwani ni
mara ya kwanza kwa kata hiyo kupata ugeni kutoka katika ngazi ya juu ya
serikali na kumuomba Mpina kupitia Wizara yake kutatua changamoto
inayoikabili kata hiyo la josho la kuoshea ng’ombe ambapo Waziri Mpina
amehaidi kuitatua.
Katika hatua nyingine Waziri
Mpina ametembelea mapori ya Burigi yaliyopo wilayani Biharamulo ambapo
ameupongeza uongozi wa mkoa kwa uporasheni iliyofanyika ya kuondoa
mifugo katika mapori tengefu na hifadhi za misitu ambapo amewashuhudia
wanyama pori ambao tayari wamerejea katika mapori hayo huku mkuu wa
wilaya hiyo Bi SAADA MALUNDE Akiwataka wananchi wa wilaya hiyo kutoa
ushirikiano katika zoezi la kuondoa mifugo.
Aidha, Mpina amewataka wakuu wa
Mikoa ya mipakani kuwasilisha kwake taarifa ya uondoshwaji wa mifugo
katika mikoa yao mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la oparesheni
ondoa mifugo.
Waziri MPINA amemaliza ziara yake
ya siku mbili mkoani kagera kubwa akiwa ameagiza mifugo yote
iliyokamatwa kutoka nje ya nchi itaifishwe na kupigwa mnada haraka sana
kwa mujibu wa sheria.
EmoticonEmoticon