Bw,Patrick Fata ambaye ni Mhelimishaji kutoka BOT akielekeza na kutoa elimu namna ambavyo unaweza kutambua Noti bandia.
Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Chato Shaaban Ntarembe.
Maafisa
wa BOT wakifuatilia maelezo ya Meneja Msaidizi wa Idara ya Uhusiano wa
BOT, Vicky Msina wakati alipokuwa akielezea juu ya elimu ambayo wanaitoa
kwa viziwi.
Meneja
Msaidizi wa Idara ya Uhusiano wa BOT, Vicky Msina akielezea malengo ya
kutoa elimu ya kuwawezesha viziwi kutambua alama za usalama zilizopo
kwenye noti ili kuzitofautisha na noti bandia pindi wanapokuwa katika
shughuli zao za utafutaji.
Mwenyekiti
wa Kituo cha Sanaa na Utamaduni kwa Viziwi Tanzania (Kisuvita), Habibu
Mrope akizungumza changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo watu ambao
ni walemavu hususani wakati wanapokuwa wanakwenda kwenye huduma za
kibenki.
Bw,Patrick Fata ambaye ni Mhelimishaji kutoka BOT,akisisitiza swala la alama za fedha ambazo zinakuwepo kwenye noti.
Kifaa ambacho kinatumika kuangalizia noti bandia na ile ambayo ni ya harari.
Noti
ambazo zinakuwa zimeharibiwa zikiwa kwenye mafungu fungu lenye rangi
nyekundi ni elfu kumi na yenye rangi ya blue ni elfu tano.
NA JOEL MADUKA,CHATO.
Benki
kuu ya Tanzania (BOT)imekutana na kundi la watu wenye ulemavu wa
kutokusikia na wale ambao hawaoni Wilayani Chato lengo likiwa ni
kuwapatia na elimu ya utambuzi wa Noti bandia Wilayani humo.
Akizungumza
kwenye semina ambayo imefanyika kwenye ukumbi wa KKKT Wilayani
Humo,Meneja msaidizi wa idara ya uhusiano wa BOT, Vicky Msina alisema
elimu wanayoitoa imelenga kuwawezesha viziwi kutambua alama za usalama
zilizopo katika noti ili kuzitofautisha na noti bandia wanapokuwa katika
shughuli zao kwani mtu yeyote akikutwa na noti bandia ni kosa la jinai,
hivyo wanawapa mafunzo ili wasikumbwe na kadhia hiyo.
“Ni
muda sasa walituomba kuwapa mafunzo na hii ni kutokana na wengi wao
kutokujua noti bandia wamekuwa wakijikuta wanabambikiwa na pia wanapo
kwenda benki kupeleka fedha zao wahudumu huwadharau na wakati mwingine
kwa wale wanao kwenda kuchukua fedha hupatiwa noti chafu jambo ambalo
lilitusukuma kuwaelimisha juu ya hatua za kufuata ilikupatiwa haki zao
za msingi kwenye huduma hizo,”alisema Msima.
Mwenyekiti
wa Kituo cha Sanaa na Utamaduni kwa Viziwi Tanzania (Kisuvita), Habibu
Mrope alisema kuna tatizo kubwa la kutotambua noti bandia kwa Walemavu
hali ambayo imechangia kuwarudisha nyuma kwani wanapokutwa na noti hizo
huchukuliwa hatua za kisheria.
Hata
hivyo kutokana na tatizo hilo Mkuu wa wilaya ya Chato Shaaban Ntarambe
aliwaahidi watu ambao wanamatatizo ya kutokusikia kufunguliwa kwa shule
ambayo itawasaidia kujifunza lugha za alama kwania ya kuboresha
mawasiliano kwenye jamii.
“Idadi
ya wilaya yetu kuna Viziwi 347 ambapo ni sawa na asilimia 90 ya watu
wenye ulemavu wa kusikia hawajui lugha za nyakati upekee idadi hii ni
kubwa sana ni lazima Serikali ifanye jitihada za kuwa kwamua watu hawa
ambapo kwa kushirikisha wadau mbali mbali, nitahakikisha ujenzi wa shule
hiyo unaanza mara moja,”alisisitiza Tarambe
Kwa
upande wake mmoja wa washirki wa semina hiyo, Issa Pastori, mkazi wa
Buziku wilayani humo alishukuru kupatiwa mafunzo hayo na kwa upande wa
suala la uanzishwaji wa shule maalum ya lugha za alama ameomba mchakato
huo uanze haraka kwani ni mkombozi kwao.
EmoticonEmoticon