Wamiliki
wote wa migodi inayofanya shughuli za uchimbaji wa madini Mkoani
Singida wameagizwa kuhakikisha kuwa hakuna vifo wa majeruhi katika
maeneo yao kutokana na uwepo wa miundombinu mibovu au uzembe wowote.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa agizo hilo alipotembelea
mgodi wa madini katika Kijiji cha Konkilangi, Kata ya Ntwike, Tarafa ya
Shelui, Wilaya ya Iramba kuona shughuli za uokoaji mara baada ya mgodi
huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa kufariki.
Dkt
Nchimbi amesema wamiliki wa migodi wanatakiwa kuwekeza katika kuboreha
miundombinu ya migodi ili wachimbaji waweze kufanya kazi katika
mazingira ambayo si hatarishi.“Madini yanatakiwa kuleta neema na kukuza
uchumi wa taifa letu na sio kuangamiza nguvu kazi na kuleta majonzi,
serikali haiwezi kukubali kupoteza vijana kutokana na uzembe wa baadhi
ya watu”, amesema.
Ameongeza
kwa kumtaka Kamishna Msaidizi wa madini kanda ya kati Sostenes Masolla
kuweka ratiba ya kutoa mafunzo kila wiki huku akitakiwa kushirikiana na
wadau mbalimbali ili wachimbaji wapewe semina na mafunzo ya juu ya
usalama wao wawapo migodini.
Dkt
Nchimbi pia amemtaka Kamishna huyo wa madini kufuatilia taaluma na sifa
zinazotumika kuchagua wakaguzi wa migodi maarufu kama ‘inspekta’ kwakuwa
wao ndio hutakiwa kwa kiwango kikubwa kuhakikisha kuwa shimo au duara
liko salama kabla ya kuruhusu uchimbaji kufanyika.
“Hawa
ma inspekta hawa wasituulie vijana kutokana na uzembe wao, unakuta
hajakagua vizuri halafu anaruhusu watu walipue baruti matokeo yake ndio
kama haya, hawa wakiwa makini ajali za kwenye migodi zitapungua sana”,
amesisitiza.Aidha Dkt Nchimbi amewataka wachimbaji na wamiliki wa migodi
kuachana na imani potofu kuwa endapo vifo vinatokea katika shimo la
mgodi hapo panakuwa na madini mengi.
Amesema
ikiwa atabaini kuwa imani hizo zinaendekezwa na kipa endapo patatokea
tena kifo katika mgodi huo basi hatasita kufunga shughuli za uchimbaji
katika mgodi huo.Kwa upande wao wachimbaji wameeleza kuwa ajali hiyo
imesababishwa na uzembe wa mgakuzi wa shimo hilo ambaye aliruhusu
ulipuaji wa baruti wakati mazingira yakiwa hayaruhusu.
Wachimbaji
hao wamemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa wamekosa amani kutokana na vifo hivyo
ambavyo kwa kiwango kikubwa vimetokana na uzembe huku pia wakilalamikia
utaratibu wa malipo yao.Mmoja wa wachimbaji hao Abuu Amiri amesema ma
inspekta hao wamekuwa wakijali maslahi binafsi badala ya kuangalia
usalama wa wachimbaji watakaoingia katika shimo hilo.
Mgodi
ujulikanao kwa jina la Sekenke 1 katika kitalu namba 1, ambapo maduara
matano yanayomilikiwa na Marijan Ramadhani na Jakobo Ntobi, yalititia
mnamo tarehe tisa Septemba na kusababisha vifo kwa wachimbaji wawili
huku mmoja tayari mwili wake ukiwa umepatikana na majeruhi watano.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na wachimbaji
alipotembelea mgodi wa madini katika Kijiji cha Konkilangi, Wilayani
Iramba kuona shughuli za uokoaji mara baada ya mgodi huo kutitia huku
watu wawili wakihofiwa kufariki. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya
Iramba Emmanuel Luhahula.
Wachimbaji
wakiendelea na shughuli za uokoaji katika Kijiji cha Konkilangi,
Wilayani Iramba mara baada ya mgodi huo kutitia huku watu wawili
wakihofiwa kufariki.
Wachimbaji
wakiwa wanatazama shughuli za uokoaji zikiendelea katika Kijiji cha
Konkilangi, Wilayani Iramba mara baada ya mgodi huo kutitia huku watu
wawili wakihofiwa kufariki.
Mmoja
wa wachimbaji Abuu Amiri akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt
Rehema Nchimbi alipowatembelea kuona shughuli za uokoaji katika mgodi wa
madini wa Kijiji cha Konkilangi, Wilayani Iramba mara baada ya mgodi
huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa kufariki.
Umati
wa Wachimbaji uliojitokeza kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt
Rehema Nchimbi alipowatembelea kuona shughuli za uokoaji katika mgodi wa
madini wa Kijiji cha Konkilangi, Wilayani Iramba mara baada ya mgodi
huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa kufariki.
EmoticonEmoticon