Sekta
ya kilimo nchini ni kitovu cha maendeleo ya viwanda kwa kutoa masoko na
malighafi za viwandani ambapo inaajiri Watanzania wengi takribani zaidi
ya asilimia 67.
Katika
utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo, Serikali inaendelea
kuimarisha mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya kilimo ikiwemo
kuimarisha masoko ya kilimo ili sekta hiyo iendelee kuwa na tija kwa
wakulimananchi na taifa kwa ujumla.
Hivi
karibuni Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ilitangaza
kufuta ada na tozo mbalimbali katika baadhi ya mazao ya biashara ili
kumpa unafuu mkulima wakati wa kuuza mazao yake.
Hatua
hiyo ni mwanzo mzuri wa kuimarisha sekta hiyo hasa wakati huu ambapo
Serikali ya Awamu ya Tano imetangaza nia yake ya kuimarisha uchumi wa
kati na viwanda.
Serikali
iliamua kufuta na kupunguza ada na tozo imedhamiria kumaliza kero na
kilio cha muda mrefu cha wakulima ambao wamekuwa wakilalamikia tozo hizo
kwa madai kuwa zinawanyonya.
Aidha,
uamuzi huo unategemea kuwapunguzia mzigo mkubwa wa malipo ambao umekuwa
ukiwaelemea wakulima hao, hivyo kuwapa unafuu mkubwa na kuwapatia
faida.
Akiwasilisha
hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2017/18, Waziri wa
Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba alizitaja baadhi ya tozo
zilizofutwa katika zao la tumbaku kuwa ni mchango wa ushirika wa mkoa,
mchango kwa ajili ya gharama za masoko ya ushirika na chama cha msingi
cha ushirika, dhamana ya benki kuu ya Tanzania na fomu ya maombi ya
leseni za tumbaku.
Ada
na tozo nyingine zilizotajwa kuwa ni kodi ya leseni ya kununua tumbaku
kavu na mbichi kiwandani, leseni ya kuuza tumbaku nje ya nchi na tozo ya
Baraza la Tumbaku.
Pamoja
na kufuta tozo na ada katika baadhi ya mazao, Serikali pia imetoa
punguzo katika zao la tumbaku ambapo kodi ya leseni ya tumbaku kavu
itakuwa dola za kimarekani 2,000 badala ya dola 4,000.
Aidha,
leseni ya kusindika tumbaku imepungua kutoka dola za kimarekani 10,000
hadi 5,000 ambapo Serikali imechukua hatua hizo ili kuhakikisha wakulima
wananufaika na kilimo wakiwemo wakulima wadogo.
Kupitia
bodi ya mazao, Serikali itaendelea kuimarisha soko la mazao ya asili
hasa mazao ya jamii ya mikunde ili kukidhi mahitaji ya zao hilo katika
soko la India na zao la muhogo kwa ajili ya soko la China.
Tozo
na ada nyingine zimepunguzwa katika zao la kahawa, ambapo ada ya leseni
ya ghala la kahawa, leseni ya kukoboa kahawa, kuuza nje ya nchi kahawa
iliyosindikwa na leseni ya kununua kahawa kwa kampuni na vyama vya
ushirika zimefutwa.
Tozo
nyingine zilizopunguzwa kwenye zao la kahawa ni ya fomu ya kuomba
leseni ya kuuza kahawa ya kijani, leseni ya ghala na leseni ya kukoboa
na kusindika kahawa pia zimefutwa.
Kwa
upande wa zao la sukari jumla ya ada 17 zimefutwa ambazo baadhi ni ada
hizo ni ya leseni ya uingizaji sukari ya viwandani, ada ya leseni kamili
ya uzalishaji sukari mkubwa na mdogo, leseni ya muda ya uzalishaji
sukari uwekezaji mdogo, leseni ya marudio kila baada ya miaka mitatu na
ada ya leseni ya kuchakata miwa.
Vilevile
ada ya kusajili kwa waagizaji wakubwa na wa kati, na ya
wafanyabiashara wa sukari ya matumizi ya kawaida ikiwa ni pamoja na ada
ya kupata kibali cha kuingiza sukari ya viwandani zimefutwa pia.
Mazao
ya pamba, chai na korosho pia yamo katika kufutiwa tozo na ada. Hii ni
pamoja na tozo ya kituo cha kununulia pamba katika ngazi ya Halmashauri
na tozo ya maendeleo ya elimu katika Halmashauri ya Meatu.
Katika
zao la chai, tozo kwa ajili ya gharama ya uendeshaji wa vyama vya
wakulima na ada ya leseni ya kununua korosho zimefutwa, ambapo wakulima
na wafanyabiashara watapata unafuu wakati wa kuuza mazao yao.
Katika
kuhakikisha wakulima wanaendelea kunufaika na kilimo, Serikali pia
imefuta baadhi ya ada katika pembejeo ya mbolea ambapo wafanyabiashara
wa mbolea hawatalipia usajili wa mbolea, ada ya leseni na usajili wa
mzalishaji.
Akizungumzia
kufutwa kwa tozo na ada hizo, wakati wa maonesho ya kilimo (Nanenane)
yaliyofanyika Kitaifa hivi karibuni katika viwanja vya Ngongo mkoani
Lindi, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole
Nasha alisema kuwa Serikali ilifikia hatua hiyo baada ya kupokea
malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa tozo hizo hazikulenga kuwakwamua
wakulima katika wimbi la umaskini badala yake ziliwazidishia umaskini.
Aliendelea
kusema kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliamua kufuta tozo na ada
hizo ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha inaondoa
vikwazo vyote vilivyokuwa vikiwakabili wakulima ili kuwainua na kukuza
uchumi.
Aidha,
Serikali za Mitaa zimeagiza kuacha kutoza ushuru kwa mazao
yanayosafirishwa kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine ili kurahisisha
na kuwapunguzia wakulima mzigo wa kulipa kodi.
Kutokana
na kupunguza kodi, tozo na ada mbalimbali katika mazao hayo ya
biashara wakulima wanatakiwa kuitumia nafasi hiyo kwa manufaa yao kwa
kujiongezea faida ikiwa ni pamoja na kuzingatia kilimo bora chenye tija
kwa ajili ya kujipatia mazao bora yanaweza kukabiliana na soko la
ushindani ndani na nje ya nchi hatua itakayowasaidia kufikia uchumi wa
kati ifikapo 2025.
EmoticonEmoticon