Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe .
Luhaga Mpina kushoto akimsikiliza Mratibu wa Kanda ya Mashariki kutoka NEMC
Bwana Jafari Chimgege alipokuwa akizungumzia suala la utunzaji wa
mazingira na ukiukwaji wa sheria ya Mazingira katika eneo la Viwanda
Mikocheni jijiniDar es Salaam.
Sehemu ya taka ya vyuma chakavu katika kiwnda cha Iron and Steel Limited jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga
Mpina akiongea na vyombo vya habari baada ya ziara ya ukaguzi wa baadhi
ya viwanda jijini Dar es Salaam Leo.
NA ; EVELYN MKOKOI, DAR ES SALAAM
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
anayeshughulikia Masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amesema
Serikali haitawavumilia wawekezaji wenye viwanda wanaokiuka sheria za nchi hasa
ya uchafuzi wa mazingira.
Mpina ameyasema hayo leo alipokuwa katika ziara ya kikazi jijini Dar Es Salaam ya uzingatiaji
wa sheria ya Mazingira alipotembelea eneo la viwanda mikocheni katika kiwanda
cha Iron and Steel Limited, BIDCO limited na Basic elements Limited.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo
Mpina alisema yeye na team yake katika ziara hiyo wamebaini
uvunjifu mkubwa wa sheria katika uchafuzi wa mazingira kwenye viwanda hivyo na
kiwanda cha Iron Steel na Basic Limited , kila kimoja kimetozwa faini ya sh.
Milioni 10 inayotakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili na kutakiwa kufanya
marekebisho ya mfumo.
Katika kiwanda cha utengenezaji
bidhaa ya Unga wa ugali cha Basic
Element alisema kwa kushirikiana na wataalamu wa mazingira wamebaini wamiliki
wa kiwanda hicho wamekiuka kanuni kwa kuziba mfereji wa maji taka.
“Kilichofanyika hapa hakikubaliki na
hakiwezekani kufumbiwa macho walichokifanya wamiliki wa kiwanda hiki ni
ukiukwaji wa sheria na wamesababisha wananchi wengi waishi katika mazingira
hatarishi haiwezekani kuziba mfereji mkubwa kama huu ambao maji taka mengi
yalitakiwa kusafiri ikiwemo kutoka viwanda vingine ni hatari,”alisema.
Alisema awali kabla ya kiwanda hicho
kujengwa ulikuwepo mfereji huo hivyo ni vyema wenye kiwanda wangeshirikiana na
Baraza la Mazingira NEMC kutafuta njia bora ya maji hayo kusafirishwa Kwenye
mfumo wa majitaka wa DAWASCO bila kuathiri mazingira.
“Lengo ni kukomesha kabisa uchafuzi wa mazingira kwa
wenye viwanda utokanano na majitaka na moshi viwandani , kwani una athari kubwa
kwa mazingira na viumbe hai vingine.” Alisisitiza Mpina.
Kwa upande wake Mratibu wa Mazingira Kanda ya Mashariki kutoka Baraza la taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
NEMC Bw. Jaffar Chimgege alisema kuwa katika kiwanda cha Iron Still Limited
imebainika kuwa wafanyakazi wa kiwanda
hicho hawana vifaa vya vya usalama
kazini kitendo ambacho kinatishia afya zao.
Aidha alisema kiwanda hicho kinatakiwa kurekebisha mfumo wa utoaji moshi kiwandani hapo pamoja na kupima moshi kiwango cha ubora wa hewa pamoja na kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa mazingira ya robo mwaka NEMC, Pamoja na kuajiri Afisa mazingira atayewashauri kuhusu masuala yote ya mazingira.
Aidha alisema kiwanda hicho kinatakiwa kurekebisha mfumo wa utoaji moshi kiwandani hapo pamoja na kupima moshi kiwango cha ubora wa hewa pamoja na kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa mazingira ya robo mwaka NEMC, Pamoja na kuajiri Afisa mazingira atayewashauri kuhusu masuala yote ya mazingira.
Baadhi ya wakazi wa Eneo la Mikocheni
‘B’ akiwemo Kanali Mstaafu wa Jeshi Bw. Lameck Meena alisema kuwa kama mkazi wa
eneo hilo ana mashaka na wasi wasi wa afya ya familia yake na mazingira kwa
ujuma kutokana na sababu kuwa moshi majitaka na vumbi linatoka katika baadhi ya
viwanda hivyo siyo rafiki na kushauri wamiliki wenye viwnda hivyo kukaa karibu
na wataalamu kuona namna ya kuweza kutatua changamoto hizo na kunusuru maisha
ya wakazi na mazingira
EmoticonEmoticon