- Mkuu wa Kitengo cha 'Trade Finance' wa Benki ya NMB, Linda Teggisa akimweleza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo kuhusu huduma mbalimbali ambazo zinatolewa na Benki ya NMB alipotembelea banda la banki hiyo kwenye maonesho ya 41 ya Saba Saba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
- Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo (kulia) akiuliza jambo kwa Mkuu wa Kitengo cha Trade Finance wa Benki ya NMB, Linda Teggisa (kushoto) wakati alipotembelea banda la Benki ya NMB kwenye maonesho ya 41 ya Saba Saba.
NAIBU Katibu
Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo ameipongeza Benki ya NMB kwa
kuanzisha akaunti ya Fanikiwa kwani ina lengo la kuwagusa watu wa kipato
cha chini ambao ndiyo sehemu kubwa ya wananchi wa Tanzania. Mpogolo
ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la benki ya NMB kwenye maonesho
ya Saba Saba ambapo alipata fursa ya kupata elimu kuhusu bidhaa na
huduma mbalimbali zinatolewa na benki hiyo kubwa nchini.
Aidha,
alisema kuwa akaunti hiyo ni nzuri kwa sababu ni mahususi kwa ajili ya
wafanya biashara wadogo wadogo wakiwemo mama lishe, wakaanga chips,
wauza magenge n.k ambao ni sehemu kubwa ya Watanzania. Akaunti hii pia
inamwezesha mfanyabishara kutambulika kama mteja mfanya biashara, atakua
mwanachama kweye klabu za biashara za NMB (NMB Business Club),
itamwezesha kupata mkopo mpaka milioni thelathini, ina gharama nafuu za
uendeshaji na ni rahisi kuifungua kwani haihitaji nyaraka nyingi. Lakini
pia mteja anaweza kupata huduma katika matawi zaidi ya 200 ya NMB
yaliyoenea nchi nzima.
“Akaunti
ya Fanikiwa inalenga kuwasaidia wafanyabiashara wadogo ili waweze
kukuza mitaji na kuendeleza kipato chao; mtu anapopata nafasi ya kupata
mkopo ni njia ya kuongeza kipato cha familia na ndivyo uchumi wa taifa
unavyoweza kujengwa, Mimi niwapongeze benki ya NMB kwa kuanzisha akaunti
hii na niwahamasishe Watanzania watumie fursa hii kuweza kuongeza
kipato kwa ajili ya maisha yao na waweze kukuza uchumi wa nchi yetu,”
alisema Mpogolo.
Vilevile,
Mpogolo aliwaasa wananchi wasiogope kuchukua mikopo kwenye mabenki ili
waweze kuongeza kipato, “Ni jukumu la kila mtu kumuhamasisha mwenzake
aone benki ni mahali anapoweza kupata fursa za kujikomboa kiuchumi,
kuendeleza ustawi wake kwani mambo kama haya zamani hayakuwepo ambayo
yanagusa watu wa hali ya chini.”
“Binafsi
jambo lililonigusa ni kuanzishwa kwa akaunti ambayo inagusa watu wa
kipato cha chini, naona kwamba Benki ya NMB inakwenda kuwa mkombozi wa
watu wanyonge kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais na serikali
yake ya kuona wananchi wa kawaida na wao wanaboresha uchumi wao.”
______________________________ ______________________________ _______________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
EmoticonEmoticon