Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan amezipongeza juhudi zinazofanywa na taasisi ya Merck ambayo ni
kampuni inayoongoza katika sayansi na teknolojia ambayo
imelenga kushughulikia masuala uwezeshwaji wa wanawake na huduma za
afya akisema kwamba wamekuja nchini kwa wakati mwafaka
Wakati
wa mkutano maalum kati ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Merck Foundation Makamu wa Rais alisema
kuwa Merck Foundation inakaribishwa na serikali inatarajia
kushirikiana na taasisi hiyo inayoheshimika na iliyo makani
katika kuwezesha wanwake , vijana, huduma za afya na sayansi.
Tunatambua
mchango unaotolewa na Merck Foundation katika kujengea uwezo huduma
za afya barani Afrika na tunakaribisha shughuli zake nchini Tanzania,
hususani katika kampeni zinazolenga kuuongezea umma uelewa kuhusu
ugumba.
Makamu
wa Rais aliongeza, “Mimi binafsi nitafanya kazi na Merck katika
kuwawezesha wanawake walio na uwezo duni kijamii na kiuchumi kote nchini
Tanzania na sehemu nyingine duniani ili kujenga utamaduni mpya katika
kuheshimu na kumtambua wanawake kama sehemu ya wanajamii
wanaozalisha wawe ni kinamama na hata wasio wazazi.”
Merck
Foundation hali kadhalika imejikita katika ushirikiano wa muda mrefu
na serikali ya Tanzania katika kuijengea uwezo katika huduma za afya na
kuboresha kufikiwa kwa ubunifu na masusluhisho yaliyo katika
uwiano kote nchini ikiwa ni sehemu ya program za uwajibikaji kwa jamii
barani Afrika.
“Merck
Foundation itatilia mkazo katika uwezeshwaji wa wanawake walio na
tatizo la ugumba kupitia upatikanaji wa taarifa, uelewa, afya, kubadili
mitazamo na kuwewawezesha kiuchumi kote nchini kupitia kampeni ya
Merck ya Zaiidi ya mama,” alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Merck, Dk.
Rasha Kelej.
Kampeni
hiyo ambayo inatoa msukumu kwa vyombo vya habari na wadau
wengine kuchpisha na kuwasilisha mada kwa njia ya mtandao, video na
vipindi vya redio kuhusu masuala yanayohusu ugumba ilizinduliwa nchini
Tanzania Juni mwaka huu. Washindi katika kampeni hiyo wanatarajiwa
kuondoka na zawadi ya fedha kuanzia dola 1000 hadi dola 5000.
“Tatizo
la ugumba barani Afrika ni kubwa, inakadiriwa kuwa mtu mmoja kati ya
kila watu wane walio na umri wa kuzaa anasumbuliwa na tatizo la ugumba,
na takribani asilimia 85 wale walio na tatizo la ugumba linatokana na
ukosefu wa tiba kwa ugonjwa ambao unaweza kutibika, hivyo kuongeza
uelewa kuhusu kuzuia hali hiyo kupiti vyombo vya habari vya ndani na
mitandao ya jamii ni hatua muhimu.”, alisema Dk. Rasha Kelej’’
Aliongeza,
“Kujenga uelewa kuhusu ugumba kwa wanaume kwani ugumba una athari
sawa kwa wanaume na wanawake, lakini wamekuwa ndio wanaolaumiwa peke
yao, wanatengwa na kudhalilishwa ndani ya jamii zao. Kampeni
itashughulikia mada hizi na kutoa msukumo kwa wanaume kujadili kwa
uwazi tatizo lao la ugumba na kushirikiana katika safari ya kutambua
ugumba na matibabu ya wake zao.”
Kwa
upande mwingine Merck foundation itajikita zaidi katika kugharamia
mafunzo kwa wataalamu wa afya kwenye maeneo ya saratani kwa watoto
(paediatric oncology) katika programu za udhamini nchini India, Ulaya na
katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwa madaktari wa Tanzania ili kuboresha
upatikanaji wa huduma zote zinahusu saratani.
Hivi
karibuni Merck ilizindua Tuzo ya Kuvitambua Vyombo vya Habari kupitia
kampeni yake ya “Zaidi ya Mama” ili kuwatuza waandishi wa habari na
wanafunzi wanaosomea uandishi wa habari katika eneo la Afrika Mashariki
ambao watakuwa wamefanya vizuri katika kuandika habari zinazoelewesha,
kuelimisha na kuhabarisha ambazo zitaweza kujenga jukwaa la
majadiliano kuhusu ugumba ndani ya Afrika. Hafla ya kutoa tuzo hizo
inatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu 2017.
Lengo
la tuzo hizo ni kujenga uelewa kuhusu mchango muhimu ambavyo vyombo
vya habari vinaweza kuutoa katika kuondo unyanyapaa uliojikita katika
tatizo la ugumba. Hali kadhalika zinalenga utamaduni mbovu wa
kuwabagua na kuwadhalilisha wanawake na papo hapo kuuelimisha
umma kuhusu kuzuia ugumba, kuisimamia hali hiyo na ugumba kwa wanaume.
Nyongeza katika kampeni hiyo ni kwamba inalenga kutoa msukumo kwa
wanawaume kujadili hali yao ya ugumba kwa uwazi, kuwasaidia wake zao
katika safari zao za kupimwa na kutibiwa.
Kufahamu zaidi kuhusu program za Merck Foundation na mafunzo yao pamoja na fursa za udhamini. Tafadhali tembelea tovuti yao www.merck-foundation.com na www.merckmorethanamother. com
EmoticonEmoticon