Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla ameendelea na ziara yake ya kikazi ya kukagua
huduma za Afya ‘Imarisha Afya’ katika Zahanati, Vituo vya Afya na
Hospitali mbalimbali kwenye mikoa ya Rukwa, Katavi pamoja na Tabora.
Akiwa
katika mkoa wa Rukwa, Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea Hospitali ya
Sumbawanga ambayp ni ya Mkoa wa Rukwa na kujionea mambo mbalimbali huku
akiwapongeza kwa namna walivyoboresha huduma zao ikiwemo ile ya Maabara,
Chumba cha upasuaji na huduma zingine ambapo aliwaagiza kuhakikisha
wanakuwa na hakiba ya kutosha ya damu salama kwa ajili ya dharura kwa
wagonjwa wa ukanda huo.
Mbali
na Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, pia aliweza kutembelea kituo ca Laela
ambapo pia mbali ya kujionea utendaji kazi wa kituo hicho alipongeza
juhudi za Mbunge wa jimbo la Kwera, Mh. Ignas Alloyce Malocha kwa
kushirikiana na wananchi wake katika masuala ya huduma za Afya.
Ziara hiyo katika
mkoa wa Rukwa, aliweza kumalizia katika Kituo cha Afya Wampembe
kilichopo Wilayani Nkasi ambapo alijionea shughuli mbalimbali ikiwemo
huduma za Upasuaji hata hivyo aliutaka uongozi wa kituo hicho ambacho
kipo mwambao wa Ziwa Tanganyika kuhakikisha wanakamilisha mifum ya maji
safi na salama ndani ya kituo pamoja na kuboresha huduma za Maabara na
usafi kwa ajumla.
Akiwa
katika Mkoa wa Katavi, Dk. Kigwangalla aliweza kufanya ziara ya
kushtukiza kituo cha Afya Inyonga,kilichopo Mlele majira ya Saa Sita
mchana na kuweza kukagua maeneo mbalimbali ikiwemo Chumba cha Maabara,
Chumba cha Upasuaji na wodi ya akina mama wanaosubiria kujifungua.
Hata
hivyo, Dk. Kigwangalla amemtaka Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo hicho
kumuandikia maelezo juu ya kutokuwepo kwa watoa huduma kwenye jingo la
chumba cha upasuaji na eneo la wodi ya akina mama wanaosubiria
kujifungua kwani licha ya kufika hapo hakukuta mtoa huduma hata mmoja
kwa wakati huo hali ambayo inaweza kuleta hatari.
“Nataka
kupata maelezo kwa maandishi. Kwa nini hakukua na watoa huduma ndani ya
Chumba cha upasuaji na kule kwa wodi ya wamama wajawazito. Nilifika
kuwakagua kwa upande wa Maabara nimekuta safi mumeweza kuboresha huduma
na mumezingatia maelezo yangu niliyoyatoa kipindi nilichofika kukagua
mwaka jana. Lakini pia hali niliyoikuta katika maeneo hayo
niliyotembelea bila kuwakuta wahusika hii ni hatari nitahitaji maelezo
ya kimaandishi” alieleza Dk. Kigwangalla wakati akitoa maagizo kwa Kaimu
Mganga Mkuu wa kituo hicho.
Aidha,
akiwa katika mkoa wa Tabora, aliweza kutembelea eneo la jengo
linalojengwa Hospitali ya Wilaya ya Uyui na baadae aliweza kumalizia
ziara yake katika Zahanati ya Isikizya ambapo aliagiza Mkurugenzi wa
Wilaya ya Uyui kuhakikisha wanatenga bajeti pamoja na kushirikiana na
nguvu za wananchi na mbunge wa jimbo hilo wanajenga majengo ya kulazwa
wagonjwa, chumba cha upasuaji, maabara na miundombinu mingine ili
Zahanati hiyo ije kupanda na kuwa Kituo cha Afya kwani kinahudumia eneo
kubwa katika mji huo wa Isikizya ambayo hipo ndani ya Makao makuu ya
Wilaya hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akikaguachumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa
Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua Maabara ya Mkoa wa Rukwa
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akikaguachumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa
Rukwa
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa viongozi wa Hospitali ya Mkoa
wa Rukwa
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akiingia chumba cha Wodi ya wanawake kituo cha
Afya Laela Mkoa wa Rukwa
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akielekea kukagua Maabara ya Kituo cha Afya Laela
Mkoa wa Rukwa
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Mh. Saidi Mtanda akihutubia wakati Naibu Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi
Kigwangalla alipotembelea kituo cha Afya Wampembe Mkoa wa Rukwa
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua kitanda ndani ya chumba cha kujifungulia
katika kituo cha Afya Wampembe Mkoa wa Rukwa
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akitembelea kituo cha Afya Wampembe, Mkoa wa
Rukwa. kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mh. Said Mtanda
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua mfumo wa maji unaoingia kituo cha Afya
Wampembe, kutokea Ziwa Tanganyika, Mkoa wa Rukwa
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua chumba cha upasuaji mdogo cha Kituo cha
Afya Nkasi alipotembelea hapo majira ya saa mbili usiku, Mkoa wa Rukwa
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua eneo litakalojengwa majengo ya utanuzi wa
kituo hicho cha Afya ambapo kikikamilika kinatarajia kuwa Hospitali ya
Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo ya maendeleo ya jengo
linalojengwa kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Uyui, Mkoani Tabora,
kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini Mh. Almasi Maige
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua jengo litakalojengwa Hospitali ya Wilaya
ya Uyui, Mkoani Tabora.
Jengo linaloendelea kujengwa kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Uyui
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua ndani ya Maabara ya Kituo cha Afya
Inyonga, Mlele, Mkoani Katavi
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh.
Dk.Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni Kituo cha Afya
Inyonga, Mlele, Mkoani Katavi
EmoticonEmoticon