Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, kulia
akimkabidhi nyaraka halali za Benki ya NMB zinazoonyesha kuingizwa kwa
fedha za mshindi wao Sospeter Muchunguzi pichani kushoto jumla ya Sh
Milioni 10 alizoshinda katika Bahati Nasibu yao ya Ijue Nguvu ya Buku,
droo iliyochezeshwa Jumapili. Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini
Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
MSHINDI wa droo ya saba ya Sh
Milioni 10 kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Sospeter
Muchunguzi, amekabidhiwa fedha zake huku akisema kuwa kuogopa kucheza Biko ni
dalili ya kukaribisha umasikini.
Muchunguzi aliyasema hayo
jana katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam wakati anakabidhiwa fedha zake na
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage.
Akizungumza kwa msisitizo
mkubwa, Muchunguzi mwenye ndoto za ujasiriamali alisema kwamba watu wote
waliofanikiwa katika maisha yao walithubutu katika mambo waliyokusudia
kuyafanya, hivyo ni budi kila mmoja kupita njia hiyo.
Sospeter Muchunguzi katikati akisaini nyaraka za benki ya NMB kwa ajili
ya fedha zake kuingizwa kwenye akaunti yake katika benki hiyo jana baada
ya kuibuka kidedea katika droo ya Biko ya Sh Milioni 10. Kulia ni
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko Grace Kaijage na kushoto ni Afisa wa
NMB.
Alisema uhakika wa kushinda
ni mkubwa ikiwa mtu ameamua kweli kuingia katika sekta ya michezo ya
kubahatisha, hususan mchezo wa Biko ambao hata uchezaji wake upo wazi na hakuna
dalili zozote za kudanganya washindi.
“Nilipoona utaratibu wa Biko
ni mzuri nikathubutu kucheza huku nikiamini kwamba endapo naweza kuibuka na
ushindi naweza kusogea katika hatua moja kwenda nyingine hivyo Watanzania
wenzangu hakuna haja ya kuogopa ili tusonge mbele.
“Nimefurahi kupata fedha hizi
kutoka Biko maana hata uchezaji wao kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa
kufanya miamala kwenye simu za Tigo, Vodacom na Airtel kwa kuandika kuingiza
namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumbukumbu namba ya 2456 ni rahisi hali
inayoweza kumfanya kila mtu amudu kucheza mahala popote na wakati wowote,”
Alisema Muchunguzi.
Naye Grace Meneja wa Huduma
kwa Wateja wa Biko, aliwataka Watanzania kila pembe za nchi kucheza kwa wingi
ili wajiwekee mazingira ya kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000,
10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazotoka kila
wakati, huku pia donge nono la Sh Milioni 10 likitolewa katika droo ya Jumatano
na Jumapili.
“Lengo letu ni kutoa zawadi
nono kwa kila mshindi wetu, hivyo umnachotakiwa kufanya ni kucheza Biko kwa
wingi kwa kununua tiketi kuanzia Sh 1000 na kuendelea ili mshinde, maana kucheza
mara nyingi zaidi ndio njia ya kufanikisha ushindi,” Alisema Grace na kuongeza
kuwa tiketi moja inatoa nafasi mbili, ikiwamo ya ushindi wa papo kwa hapo
pamoja na nafasi ya kuingia kwenye droo ya kuwania Sh Milioni 10.
Kwa mujibu wa Grace, washindi
wao wanaoshinda zawadi za papo kwa hapo wanatumiwa fedha zao kwa kupitia simu
walizocheza na wale wa droo kubwa wakikabidhiwa katika benki ili kuleta usalama
wa fedha wanazotoa kwa washindi wao.
EmoticonEmoticon