ZIARA YA KATIBU WA KAMATI MAALUM YA NEC IDARA YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA, MHANDISI HAMAD MASAUNI VISIWANI ZANZIBAR

March 04, 2017
 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar , Mhandisi Hamad Masauni,  akizungumza na vyombo vya habari katika eneo
la Mwanyanya Mikoroshini  lililopo mkoa  wa Mjini Magharibi ambalo matendo ya uhalifu
ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji
hufanyika hapo ambapo ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana
na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya
sheria
 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia
jeraha la mmoja wa wananchi wa eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa
Mjini Magharibi, ambaye wiki chache zilizopita alijeruhiwa na mapanga na watu
wanaofanya matendo ya uhalifu katika eneo hilo
 Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman
Khamis Juma, akizungumza na vyombo vya habari juu ya hatua zilizochukuliwa na
Jeshi la Polisi kudhibiti matukio ya uhalifu katika  eneo la Mwanyanya
Mikoroshini lililopo mkoa huo, wakati wa ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya
NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo
pichani) kutembelea maeneo sugu ya uhalifu.
 Katibu  wa Kamati Maalum  ya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na  Mkuu  wa  Upelelezi Mkoa  wa  Mjini Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma (kushoto), baada ya kutembelea eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa huo  ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji  hufanyika  ambapo Katibu huyo wa NEC  ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ally Kitole, akimueleza Katibu  wa Kamati Maalum  ya NEC
Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni baadhi ya hatua walizochukua katika kupambana na uhalifu unaoatokea eneo la Mwanyanya Mikoroshini.
Picha na Abubakari Akida

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »