Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji
Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo
mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi mine na si vinginevyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama Salma Kikwete mara
baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa
Ng’apa uliopo Mkoani Lindi. Pia Mama Salma Kikwete amemshukuru Rais Dkt.
Magufuli kwa kumteua kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge mteule
Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika
karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ng’apa mara
baada ya kutembelea mradi wa Maji wa eneo hilo ambao unasuasua
kukamilika. Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa Mkandarasi kampuni
ya Overseas Infrastructure Alliance Private Limited ya India
kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa mradi huo na sio kuleta
visingizio.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ikulu ndogo Mkoani Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza
mazungumzo yake na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) katika Ikulu ndogo Mkoani Lindi. Wakwanza kushoto ni Kiongozi wa
Wakurugenzi hao Lekhethe Mmakgoshi kutoka Nchini Afrika Kusini na
Wakwanza kulia ni Mkurugenzi mwingine wa (AfDB) Dkt.Nyamajeje Weggoro
ambaye ni Mtanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi wa Wakurugenzi
hao kutoka (AfDB) Lekhethe Mmakgoshi mara baada ya kumaliza mazungumzo
na Bodi hiyo ya Wakurugenzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mmoja wa
Wakurugenzi wa (AfDB) Dkt.Nyamajeje Weggoro mara baada ya kumaliza
mazungumzo na Bodi yao Ikulu ndogo mkoani Lindi.
Sehemu ya Mradi wa Maji wa Ng’apa
mkoani Lindi ambao Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa mkandarasi
anayejenga mradi huo ili uweze kukamilika haraka.PICHA NA IKULU
EmoticonEmoticon