MZEE ALINANOSWE ANAWATAFUTA NDUGU ZAKE WALIOPOTEZANA MIAKA KUMI ILIYOPITA

March 04, 2017
 Mzee Alinanoswe Aspain Mwambapa mzaliwa wa Tukuyu Mbeya anawatafuta ndugu zake wakiwemo kaka zake na dada zake  baada ya kupotezana nao kwa Zaidi ya miaka Kumi iliyopita.

Kwa mujibu wa Mzee huyo ameuomba mtandao huu kumsaidia kuwatafuta dada zake ambao ni Eni Aspain Mwambapa anayeishi Dar es salaam,pamoja na Buni Aspain Mwambapa Mkazi wa songea kwa sasa.
Wengine ambao mzee Alinanoswe anawatafuta ni kaka zake Ismail Aspain mwambapa Pamoja na Obole Aspain Mwambapa ambao wote walipotezana Takribani miaka Kumi iliyopita.
 
Mzee huyo ameueleza mtandao huo kuwa alitengana na ndugu zake hao mwaka 2001 Chunya mbeya na kutimkia Pwani ambapo mpaka sasa anaishi huko,ambapo sasa anatamani kurejea nyumbani kwake lakini hajui jinsi gani ya kuwapata ndugu zake na sasa anaishi kwa wasamaria wema walioamua kumhifadhi.

Mzee huyo alizaliwa mwaka 1961 Tukuyu mbeya.
Kwa mweye kumjua mzee huyu atoe Taarifa kwa namba zifuatazo ili akutanishe na ndugu yake ,
Namba

0713 562954 Augustino Michael
0789682901 Lister Godfrey
0789421644 Frank Michael
0718 528632 Frank Michael
0769 56 2954 Augustino Michael.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »