Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam wakiwa katika kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 (Picha zote na Nassir Bakari)
Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha
kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kulia kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob
Kushoto ni Muweka hazina wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi Jenny Machicho, Afisa utumishi Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ally Juma Ally, na Mchumi wa Halmashauri ya manispaa ya Ubungo Yamo Wambura wakiwa katika kikao cha
kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akizungumza wakati wa kikao cha
kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 (kushoto) ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe Ramadhan Kwangaya na (kulia) ni
Mkurugenzi
wa Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
Mstahiki Meya Boniface Jacob (kushoto) katika
picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayobo
(kulia)
Mchumi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Yamo Wambura akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya matumizi ya fedha kwenye kikao cha
kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018
Na
Mathias Canal, Dar es salaam
Baraza la madiwani katika Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam kwa kauli moja limepitisha makisio ya
mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kwa kuungwa mkono na madiwani wote
waliozuru katika mkutano maalumu wa baraza hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa
waandishi wa habari na Kaimu Afisa habari na Uhusiano wa Manispaa hiyo Bi Maria
Makombe imeeleza kuwa Katika mpango huo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inakadiria
kukusanya/kupokea kiasi cha Tshs 128,611,616,805.100 ambazo zimeelekezwa katika
matumizi ya mishahara, utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na matumizi
mengineyo.
Fedha hizo zitatokana na makusanyo ya ndani
ya Halmashauri, Ruzuku kutoka serikali kuu, Michango ya wananchi na wahisani wa Maendeleo.
Aidha Halmashauri inatarajia kupokea kiasi
cha Tshs 4,233,546,143.00 kutoka TAMISEMI kwa ajili ya kutekeleza miradi ya
ujenzi wa barabara (Road Fund).
Katika fedha hizo chanzo cha makusanyo ya
ndani ni Tshs 24,006,600,000.00 ambayo ni Sawa na asilimia 26% ya bajeti,
Michango ya wananchi ni Tshs 500,000,000 Sawa na asilimia 1% ya bajeti, Mfuko
wa barabara ni Tshs 4,233,546,143.00 Sawa na asilimia 4% ya bajeti na ruzuku
kutoka serikalini na wahisani wa maendeleo ni Tshs 59,892,884,406.00 Sawa na
asilimia 69% ya bajeti.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe
Boniface Jacob akisoma makisio ya bajeti ya Halmashauri ya Manispaa hiyo ameyataja
maeneo yaliopata kipaumbele katika mpango huo kuwa ni pamoja na Kuboresha na
kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Manispaa, pamoja na Ujenzi wa ofisi za Makao
makuu ya Halmashauri ya Manispaa hiyo.
Vipaumbele vingine ni kuboresha miundombinu
ya afya,shule za msingi na sekondari, kuboresha miundombinu ya maji, mifereji,
taa za barabarani na kilimo mjini, Kuboresha hifadhi ya mazingira na ukusanyaji
wa taka, Kuimarisha ushirikishwaji wa jamii katika upangaji na utekelezaji wa
miradi ya maendeleo sambamba na Kuboresha mazingira ya wafanyabiashara
ndogondogo.
Mhe Jacob ameeleza kuwa Manispaa hiyo ya
Ubungo imejipanga kusimamia vyema uimarishaji wa mahusiano mazuri kati ya
serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine, Kuendelea kujenga
uwezo na ujuzi kwa watumishi katika utoaji wa huduma zilizo bora na zaharaka,
kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na uwazi sambamba na Kujenga uwezo kwa
viongozi wakiwemo waheshimiwa madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa katika
kusimamia shughuli za wananchi.
Katika makisio ya matumizi ya kawaida na
miradi ya maendeleo kwa 2017/2018 asilimia 72% itatumika kwa matumizi ya
kawaida na asilimia 28% itatumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Maombi maalumu yamewasilishwa kupitia bajeti
hii ambapo ni pamoja na maombi ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa Makao makuu ya
Halmashauri, Ujenzi wa Zahanati, Ununuzi wa magari, Malipo ya fidia kwa
wananchi kwa maeneo yaliyochukuliwa na Halmashauri kwa ajili ya matumizi ya
umma.
Mstahiki Meya
alieleza Dira na dhima ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kuwa ni kuwa na
jamii inayohamasika, inayokubalika ikiwa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Kwa upande wake
Mkurugenziwa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa
mkutano huoamesema kuwa Bajeti hiyo ina mambo mengi ambayo ni muhimu katika
ustawi wa Manispaa hiyo hivyo ushirikiano wa pamoja kati ya madiwani na
watumishi wa Manispaa hiyo itaimarisha mapato na uimara wa maendeleo katika
jamii kwa kuwashirikisha wananchi.
MD Kayombo
amebainisha kuwa Bajeti hiyo ina vipaumbele vingi lakini vile vilivyo muhimu
zaidi vitafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo kwani ni sehemu ya kuimarisha
nakukamilisha mipango ya mudamfupi katika Halmashauri.
Alisema kuwa makadirio
ya mwaka 2017/2018 ya Tshs 128,611,616,805.00 yana ongezeko la kiasi cha Tshs
12,565681,576.01 ambapo Bajeti hii imepanda kwa asilimia 10 ukilinganisha na
makisio ya Bajeti ya mwaka 2016/2017 ambayo yalikadiriwa kuwa ni Tshs
116,045,935,228.99.
Vipaumbele vya bajeti hii ya mwaka 2017/2018
ya Manispaa ya Ubungo vimewekwa katika sekta mbalimbali, ambapo Halmashauri
imelenga kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kutumia mfumo wa
kielektroniki, Kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kutoa huduma kwa kujenga
ofisi za Halmashauri, Kuboresha utoaji huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi
kwa wakazi, Kutoka mikopo kwa wajasiriamali, Kuboresha usafi wa mazingira na
Kuboresha miundo mbinu ya barabara, Shule na Afya.
EmoticonEmoticon