WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akisalimiana
na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, baada ya kuwasili katika kijiji
cha Kipara Mpakani kwa ajili ya kukabidhi eneo la hekali 50 kwa
wanakijiji hicho, Mkuranga, Mkoani Pwani.
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akisaini kitabu cha
wageni kabla ya mkutano na wanakijiji cha Kipara Mpakani. Kushoto ni
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akihutubia wanakijiji cha Kipara
Mpakani kabla ya Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Maghembe
kukabidhi eneo la hekali 50 kwa kijiji hicho kwa ajili ya huduma za
kijamii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akihutubia wanakijiji cha Kipara Mpakani katika mkutano huo kabla ya makabidhiano.
Mzee
wa Kijiji cha Kipara Mpakani akimshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii,
Profesa Jumanne Maghembe na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega,
kwaniaba ya wanakijiji hicho.
Wanakijiji wakimpongeza Mbunge wao, Ulega baada kufanikiwa kupewa eneo hilo la hekali 50.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) na Mbunge wa
Mkuranga, Abdallah Ulega, wakikata majani kuashiria kukabidhi rasmi
eneo hilo kwa ajili ya huduma za kijamii.
Na Mwandishi Wetu.
SERIKALI
imerejesha eneo la hekeli 50 Kwa wananchi wa kijiji cha kipara mpakani
kilichopo Kata ya Mwandege,Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ili wajenge
huduma za kijamii.
Akikabidhi
eneo hilo Waziri wa Maliasi na Utalii Profesa Jumanne Maghembe
aliwaeleza wananchi hao ambo walijitokeza Kwa wingi katika mkutano
amesema kuwa wamponge Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega kwani
amefanya jitihada kubwa za kuhakikisha Serikili inatoa Kwa wananchi eneo
hilo.
Amesema
kuwa wakati wako Bungeni mbunge huyo pamoja na baadhi viongozi wa kata
hiyo walikwenda Bungeni na kuiomba Serikali kuwapa eneo hilo ambapo
lilikuwa pori tengefu la maliasili ili wananchi wa kata ya Mwandege
waweze kujenga Masoko.Shule,na miundombinu mingine.
"Nawapa
eneo hili leo kwaniaba ya Serikali kwani najuwa Mh.rais Dkt.Magufuli
wakati wakampeni alipita hapa nakuzungumzia eneo hili hivyo tunahitaji
mjenge huduma mbalimbali na sio baadae watu wajitokeze na kusema eneo la
kwenu."amesema Profesa Maghembe.
Naye
Mbunge Ulega akizungumza katika mkutano huo amesema kuwa wananchi hao
niwastaratibu kwani.mbali na kukosa maeneo ya kujenga huduma za jamii
bado walikuwa wamekituza eneo hilo hadi leo Serikali wanapoamua kuwapa
wananchi.
EmoticonEmoticon