Na Rabi Hume, MO BLOG
Kutokana
na kuwepo na shughuli nyingi za kibinadamu ambazo zinaharibu mazingira,
watanzania nchini kote wametakiwa kuwa makini kwa kutunza mazingira
yanayowazunguka ili kuepusha matatizo ambayo yanaweza kutokea kutokana
na kushindwa kudhibiti vitendo vya uharibifu mazingira.
Rai
hio imetolewa na Balozi Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa Geneva,
Uswisi, Modest Mero katika warsha ya kujadili kuhusu kilimo na biashara
iliyoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF).
Balozi
Mero alisema kuwa nchi nyingi duniani zimekuwa na shughuli nyingi
ambazo zinaharibu mazingira hali ambayo inatishia maisha ya vizazi
vijavyo na hivyo ni vyema watanzania wakaanza kuchukua hatua kwa kutunza
mazingira ili kuepeusha athari ambazo zitajitokeza kwa miaka ijayo.
"Dunia
nzima watu wanakata miti, wanachoma majani mashambani lakini hawajui
kama kuna vitu vya muhimu wanaua ardhini, na mimi niwambie watanzania
wawe makini wasikate miti ambayo inawazunguka huo ni uharibifu wa
mazingira," alisema Balozi Mero.
Aidha
alisema kuwa kwa sehemu kubwa watu ambao wanachangia vitendo hivyo ni
wafanyabiashara na hivyo kuwataka wafanyabiashara kuacha vitendo vya
kukata miti ikiwa bado haijafika katika muda sahihi ambao wanaruhusiwa
kuikata.
"Wafanyabiashara
wanakata sana miti, lakini wajue kuwa wakikata hovyo baadae wataikosa
hiyo miti, ili mazingira yanayotuzunguka yawe mazuri inabidi kuyatunza
ila tukitumia vibaya hata vyanzo vya maji vitakauka," alisema Mero.
Nae
Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Dkt. Osward Mashindano alisema warsha hiyo ina
lengo la kuzungumzia jinsi gani kilimo, biashara, usalama wa chakula na
mabadiliko ya hali ya nchi jinsi ambavyo vinaweza kutoa matokeo mazuri
au mabaya.
Alisema
kuwa pamoja na matokeo hayo, pia wanazungumzia ni hatua gani inafaa
kuchukuliwa iwapo matokeo yanakuwa ni mazuri au mabaya ili kumsaidia
mkulima mdogo kwa jinsi gani anaweza kufaidika na kilimo chake na
kuepuka kupata hasara.
"Bidhaa
kwa sasa zinatakiwa kuongezwa thamani, bidhaa kama haijaboreshwa
haiwezi kuwa na soko zuri la ndani na hata nje ya nchi, tunataka kujua
matokeo yake yanakuwaje maana biashara inavutia kutokana na soko lake
lilivyo,
"Watu
wanatakiwa kujua matokeo kama ni mazuri wafanyaje kama wengine wanaweza
wanachangamkia fursa au kama ni mabaya wajue jinsi gani wanaweza
kupunguza athari hizo ... tunatazama hilo maana hata sera zilizopo sasa
hazisemi hatua gani ichukuliwe kama matokeo ni mabaya au mazuri,"
alisema Dkt. Mashindano.
EmoticonEmoticon