Diwani
wa kata ya Ikuza iliyopo katika Kisiwa cha Ikuza , wilayani Muleba mkoa
wa Kagera,Fortunatus Matta (Kulia) akimueleza jambo Meneja Mawasiliano
wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete alipoongozana
na wanahabari kutembelea kijiji hicho cha Ikuza.Wengine ni wakazi wa
kijiji hicho.
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) akizungumza na
wakazi wa kijiji cha Ikuza mara baada ya kutembelea jengo la Zahanati
lililojegwa na TANAPA kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya
Muleba kwa ajili ya wakazi wa kata hiyo.
Sehemu mbalimbali za Jengo la Zahanati ya kijiji cha Ikuza wilayani
Muleba lililojengwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa
ushirikiano na Halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Mzee
William Lugaga akizungumza namna wananchi wa Kisiwa cha Ikuza
wanavyopata shida katika kupata huduma ya afya hali ambayo imewalazimu
kusafiri wa kutumia mitumbwi kwenda kutafuta huduma hiyo vijiji vya
jirani .
Pelagia
Samson,mkazi wa kijiji cha Ikuza wilayani Muleba akizungumza namna
akina mama wanavyopata shida hasa wakati wa kujifungua kutokana na
kutokuwepo kwa Zahanati katika kijiji hicho ambapo baadhi yao
wamelazimika kujifungulia kwenye mitumbwi wakati wakipelekwa kupata
huduma katika kituo cha afya kilichopo kijiji cha jirani.
Baadhi
ya wakazi wa kijiji cha Ikuza wilayani Muleba wakisikiliza kwa makini
maelezo yaliyokuwa yakitolewa kwa wanahabari (hawapo pichani)
walipotembelea kijiji hicho.
Baadhi
ya Wanahabari waliotembelea kijiji cha Ikuza ,wilayani Muleba mkoani
Kagera ,wakiwa katika picha ya pamoja na Diwani wa kata hiyo Fortunatus
Matta pamoja na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) Pascal Shelutete.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,aliyekua Muleba, Kagera.
JUMLA ya Sh. Milioni 226 zimetumika kwa ajili ya
kujenga zahanati katika kijiji cha Ikuza wilayani Muleba mkoani Kagera.
Kwa mujibu wa Diwani wa kata ya Ikuza, Fortunatus
Matta ni kwamba Zahanati hiyo ilijengwa na Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA), kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Muleba na Wananchi.
Alisema ili kukamilisha ujenzi huo, TANAPA ilitoa
Sh. Milioni 101, halmashauri ikatoa Sh. Milioni 80 huku wananchi wakichangia
Sh. Milioni 22.
“Tunaishukuru sana TANAPA kwa kupitia Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha
Rubondo, ambayo inapakana na kijiji chetu kwa kuonyesha nia kusaidia mradi huu
wa ujenzi kwa ajili ya kuokoa maisha ya wananchi wetu,” alisema.
Alisema ujenzi wa jengo hilo kutaleta matumaini kwa
wananchi ambao walikuwa wanatumia kilomita 83 kwa ajili ya kufuata huduma za
afya kwenye kituo cha Afya cha Kanisa la AICT kilichopo Kasenyi.
Aidha, alisema licha ya jengo hilo kukamilika
lakini bado kumekuwa na tatizo la kupata watumishi, vifaa tiba na dawa.
Wakizungumza na waandishi wa habari, wananchi wa
kijiji cha Ikuza, wameishukuru TANAPA kwa kuwajengea Zahanati hiyo.
Mkazi wa kijiji hicho, William Lugaga alisema:
“Nashukuru Mungu, hakuna mwanamke yeyote ambaye aliwahi kuzama kwenye ziwa kwa
ajili ya kufuata huduma za afya.”
Kwa upande wake, Peragia Samson alisema wakinamama
wanapata shida sana wanatumia muda wa saa tatu kwa ajili ya kufuata huduma ya
Afya.
“Wakinamama wanajifungulia njia kabla hata ya
kufika hospitali na wengine kwenye boti,” alisema.
Naye, Kisanti Joseph alisema naona uchungu kuona
wanawake wajawazito wanapotaka kujifungua lazima wapande boti kwenda Kasenyi.
“Kuna wanawake wengine wanajifungulia kwenye
boti…hii yote ni kukosa huduma ya Afya,”alisema.
EmoticonEmoticon