Kundi
la Wanahabari wakiongozwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi
za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete (mwenye fimbo)wakijiandaa kueleke
katika maeneo wanako patikana Sokwe mtu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya
Milima ya Mahale.
Safari
ya kuwatafuta Sokwe Mtu ndani ya Hifadh ya Taifa ya Milima ya Mahale
ikaanza kwa kupita ndani ya msitu mnene ,mabonde na hata vipando .
Kundi
la Wanahabari likiongozwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi
za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete wakiwa wamevalia "Mask" kwa ajili ya
kuzuia magonjwa yanayoweza kuambukiza kati ya Sokwe na Binadamu.
Sokwe
mtu aliyepewa jina la Michio ndiye alikuwa wa kwanza kuonekana mbele ya
kundi la wanahabri waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale
iliyopo mkoani Kigoma.
Safari
ya kuwatafuta Sokwe mtu inaendana na msemo unaosema "Huwezi kumuona
Sokwe bila kutoka jasho"ili kuhamsisha wageni kuendelea kua na nguvu ya
kumuona Sokwe wakati mwingine waongoza Wageni walilazimika kuelezea vitu
mbalimbali vilivyoko katika hifadhi hiyo .
Wakati mwingine wageni walipata mahala kwa ajili ya kupumzika huku wakisikiliza milio ya Sokwe wapi inatokea.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog ,Kigoma.
EmoticonEmoticon