Vanessa
Mdee Mdee (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi (katikati), Kaimu Mkurugenzi wa
Masoko wa TTB (kushoto), Afisa Uhusiano Mkuu wa TTB Bw. Geofrey
Tengeneza na Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Bi Devota Mdachi (kulia) akijadliana
jambo na Vanessa Mdee leo walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi za
Bodi ya Utalii Tanzania.
Mwanamuziki
maarufu wa Bongo fleva nchini Tanzania Vanessa Mdee amesema yuko tayari
kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) katika kuvitangaza
vivutio vya Utalii vya Tanzania ndani nab nje ya nchi.
Mdee
ametoa ahadi hiyo alipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii leo jijini Dar
es salaam na kufanya mazungumzo na uongozi wa Bodi hiyo kuhusu namna TTB
inavyoweza kushirikiana nae katika kutangaza na utalii wa Tanzania.
Ujio
huo wa mwanamziki huyo ambaye pia ni nguli wa miondoko ya R&B, Hip
Hop, na Afro Pop ulifuatia mwaliko wa uongozi wa TTB kuomba kukutana na
kuzungumza na mwanamuziki huyo katika azma na mkakati wa TTB kuwatumia
wasanii na watu wengine maarufu nchini katika kutangaza Utalii wa
Tanzania.
Katika
mazungumzo hayo Vanessa Mdee amesema yuko tayari kufanya kazi na TTB
kwa lengo la kutangaza vivutio vya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwa
balozi wa hiari wa Utalii “ Tutaendelea kujadiliana kuona ni
namna gani nzuri tunaweza kushirikiana, na mimi niko tayari kuifanya
kazi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa Balozi wa hiari wa Utalii” alisema
Mdee.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi alielezea
kufurahishwa kweke na utayari wa Vanessa Mdee katika kuunga mkono juhudi
za TTB katika kuutangaza na kuundeleza Utalii wa ndani sambamba na ule
wa Kimataifa, na kuahidi kukamilisha haraka mchakato mazungumzo hayo na
hatimaye kusainiwa kwa makubaliano baina ya pande hizo mbili.
Katika
kutekeleza jukumu lake la kuitangaza vivutio vya Utalii Tanzania ndani
na nje ya nchi Bodi ya Utalii Tanzania imekuwa ikibuni na kutekeleza
mbinu na mikakati mbalimbali kama vile kuweka matangazo katika
televisheni za kimataifa, kutumia mitandao ya kijamii viwanja vya mipira
ya miguu, kuandaa safari za waandishi wa habari, kutumia watu maarufu
na njia nyinginezo nyingi.