RAIS DKT MAGUFULI APOKEA SHILINGI BILIONI 12 YA BAKAA YA TUME YA UCHAGUZI

June 07, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe Jaji Mstaafu
Damian Lubuva wakimsiliza Mkurugenzi wa uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima Kobwey wakati akitoa taarifa ya namna Tume ya Uchaguzi ilivyookoa kiasi cha shilingi Bilioni 12 zilizopangwa kutumika katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya Bilioni 12 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Mkurugenzi wa uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani Kobwey ikiwa ni bakaa ya tume hiyo zilizopangwa kutumika na Tume ya Uchaguzi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka 2015.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru kwa moyo wa Uzalendo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Mkurugenzi wa uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani Kobwey baada ya kupokea bakaa ya Bilioni 12 zilizopangwa kutumika na Tume ya Uchaguzi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka 2015.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »