Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
UMOJA
wa Mafundi wa Gereji wa Wilaya Kinondoni wametengeneza magari ya Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa kwa zaidi ya Sh.Milioni 42 ikiwa ni sehemu kusaidia
ofisi hiyo wafanyakazi kusafiri kutoka sehemu moja kwenda
nyingine kutoa huduma kwa wananchi.
Akizungumza
leo na umoja huo wakati wa kukabidhiwa magari hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda amesema bila ya madereva hao kutokea kuna
baadhi ya watumishi walikuwa tayari wanajiandaa kununua magari hayo.
Makonda
amesema kuwa kutengeneza magari hayo kuna baadhi ya watu walikuwa
wanaombea suala hilo lishindikane lakini mafundi wameonyesha uwezo
wao kwa kutengeneza bure ikiwa ni sehemu kuunga mkono juhudi za Rais
Dk.John Pombe Magufuli.
Amesema
wapo watu wanauwezo lakini wameshindwa kusaidia isipokuwa mafundi
wamedhubutu kutengeneza magari ya serikali kwa gharama yao wenyewe.
Makonda
amesema kuwa mafundi gereji kwa mara ya kwanza watakuwa wameandika
historia ya dunia kujitoa kwa kutengeneza magari serikali bure watumishi
wasiweze kutengeneza mazingira ya kukaa ofisini kutokana na kukosa
usafiri.
Mkuu
wa Mkoa kwa awamu ya kwanza amekabidhiwa magari manne yaliyongenezwa na
mafundi gereji yaliyo gharimu zaidi ya sh.milioni 17 na magari mengine
yatagharimu za zaidi ya sh.milioni 25 .
Amesema
safari ya magari nane kupelekwa tegeta yaliondolewa kwa Break Down na
zingine kubebwa na gari kutokana magari hayo hata tairi zake zilikuwa
haziwezi kuzunguka.
Aidha
amesema mafundi gereji ni watu wanyonge lakini wamekuwa mstari wa mbele
hivyo wanahitaji kusaidiwa kwa nguvu zote pale wanapohitaji
msaada katika serikali.
Wakati
huo huo Umoja wa Mafundi Gereji hao wamemkabidhi madawati 100 Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ikiwa kuunga kampeni ya mkuu wa
mkoa huyo ya kuchangia madawati.
Magari
ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa yaliyogharimu zaidi ya Sh.Milioni 42 za
matengenezo ikiwa ni sehemu kusaidia ofisi hiyo wafanyakazi kusafiri
kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutoa huduma kwa wananchi.
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, RC Paul Makonda leo jijini Dar Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiingia katika moja ya gari
ambayo imetengenezwa na umoja wa mafundi gereji bure ikiwa ni sehemu ya
mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na viongozi wa umoja
wa mafundi gereji ambao walikuwa wanamkabidhi magari manne
waliyotengeneza bure ikiwa ni sehemu ya mchango wao ufundi katika
serikali leo jijini Dar es Salaam.

Magari yaliyotengenezwa bure na mafundi hao
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, RC Paul Makonda leo jijini Dar Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiendesha moja ya gari ambayo
imetengenezwa na umoja wa mafundi gereji bure ikiwa ni sehemu ya mchango
wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiingia katika moja ya gari
ambayo imetengenezwa na umoja wa mafundi gereji bure ikiwa ni sehemu ya
mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitesti moja ya gari ambayo
imetengenezwa na umoja wa mafundi gereji bure ikiwa ni sehemu ya mchango
wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.