Tume ya maendeleo ya ushirika yakusudia kuvifuta vyama 1,862 vilivyokiuka matakwa ya Sheria.

May 19, 2016

US1 
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) Kuhusu makusudio ya Tume hiyo kuvifuta vyama 1862 katika daftari la vyama vya Ushirika vyama ambavyo vimekiuka matakwa ya sheria ya vyama vya ushirika No.6 ya mwaka 2013. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
US2 
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) Kuhusu makusudio ya Tume hiyo kuvifuta vyama 1862 katika daftari la vyama vya Ushirika vyama ambavyo vimekiuka matakwa ya sheria ya vyama vya ushirika No.6 ya mwaka 2013. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa na kushoto Afisa Uhusiano wa Tume hiyo Bw. Bunyanzu Ntambi.
US3 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.
PICHA NA HASSAN SILAYO- MAELEZO
……………………………………………………………………………………………………
Tume ya Maendeleo ya Ushirika inakusudia kuvifuta katika Daftari la Vyama vyaUshirika vyama ambavyo vimekiuka matakwa ya Sheria ya Vyama vya UshirikaNa.6 ya mwaka 2013.  
Kwa mujibu wa sheria, Mrajis wa Vyama vya Ushirika, kwa mamlaka aliyopewachini ya vifungu Namba 11(3), 8(2) na 100 anatakiwa kuvifuta vyama ambavyovimeshindwa kufanya kazi katika kutimiza masharti ya usajili wake. Mashartiyaliyokiukwa ni pamoja na kutokufanya Mikutano kwa mujibu wa Sheria, kutokufanya chaguzi za viongozi kwa mujibu wa Sheria, kuwa na idadi pungufu yawanachama na kushindwa kufanya shughuli zake kwa zaidi ya miezi sita, kinyumena matakwa ya  Sheria na masharti ya vyama hivyo.
Kutokana na sababu hizo, vyama vinavyokusudiwa kufutwa ni 1,862  na vitafutwabaada ya siku tisini (90) kuanzia tarehe 13 Mei, 2016 siku ambayo Tangazo la Kusudio la Kufuta vyama hivyo ilipochapishwa katika gazeti la Serikali.
Idadi ya vyama vinavyokusudiwa kufutwa katika kila mkoa ni kamaifuatavyo: Arusha vyama 83, Dar es Salaam 91, Dodoma 50, Geita 16, Iringa 74, Kagera 240, Katavi 19, Kigoma 38, Manyara 73, Mara 203, Morogoro 278, Mtwara 52, Njombe 18, Pwani 324, Rukwa 14, Ruvuma 14, Shinyanga 89, Simiyu 93, Singida 15, Tanga 77 na Lindi 1. Orodha ya vyamavinavyokusudiwa kufutwa inapatikana katika Ofisi za Ushirika za Wilaya naMikoa na katika tovuti la Tume ya Maendeleo ya Ushirika(www.ushirika.go.tz ) .
Mtu yeyote au Taasisi yenye pingamizi la msingi dhidi ya kufutwa kwa chamahusika, anatakiwa awasilishe pingamizi hilo na sababu zake katika Ofisi ya Mrajiskupitia Ofisi za Warajis Wasaidizi wa Mikoa husika ndani ya siku tisini (90) kuanzia tarehe 13/05/2016, siku ambayo tangazo la kufutwa kwa vyama hivyolilipotangazwa katika gazeti la Serikali.
Umma unataarifiwa kwamba zoezi la kufuta Vyama vya Ushirika ambavyohaviendeshwi kwa mujibu wa Sheria ni endelevu na kwa ajili hiyo viongozi nawanachama wa vyama vya Ushirika na Maafisa Ushirika wanaagizwa kuhakikishakwamba Vyama vya Ushirika katika maeneo yao viendeshwe kwa kuzingatiamatakwa ya Sheria ya Vyama vya Ushirika ili kuepuka vyama vyao kufutwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »