Meneja
utetezi wa Oxfam Tanzania, Eluka Kibona amesema uelewa wa wanawake katika
kumiliki ardhi na kufuatilia haki zao za ardhi unaongezeka siku hadi
siku nchini na kuondoa ile dhana kwamba wanawake wako nyuma katika
shughuli za maendeleo.
Bi Eluka
ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Blogs za Mikoa kuhusu namna taasisi
binafsi zinavyotetea harakati za wanawake katika kumiliki ardhi hapa
nchini na kujiendeleza kiuchumi ambapo amesema kwa kulinganisha miaka 10
iliyopita na sasa, wanawake kwa sasa wamekuwa na muamko zaidi wa
kupambana na changamoto za umiliki wa ardhi wanazokutana nazo.
''Sisi
tunaunga mkono harakati na jitihada za kuleta usawa kati ya wanaume na
wanawake mjini na vijijini na hii ni baada ya kutambua kuwa matatizo ya
umiliki wa ardhi kwa wanawake wa mjini na vijijini yako sawa kutokana na
mfumo ulivyo katika jamii.''Ameeleza Bi Eluka.
Mmoja wa wanawake (Kulia) akipokea hati yake ya kumiliki ardhi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster katika kijiji cha Gongoni wilayani Kilosa.
''Kuna madai
ya ardhi ambayo wanawake wanakumbana nayo katika jamii kwa kudhulumiwa
na wengine kwa kunyimwa haki zao za msingi hivyo tunawasaidia katika
kuwawezesha kutambua namna ya kupigania haki zao.''Amesisitiza Bi Eluka.
Kuhusu siku
ya wanawake duniani ambayo huazimishwa kila Machi 8 kila mwaka, Bi Eluka
amesema Oxfam Tanzania imejipanga kufanya maadhimisho katika mkoa wa
Mtwara ili kuunga mkono jitihada za wanawake katika kujikwamua na mifumo
kandamizi hapa nchini na kujiendeleza kiuchumi.
Kwa mujibu
wa Bi Eluka, Oxfam imewezesha wanawake wengi kuweza kupata haki zao
katika mikoa mbalimbali nchini na baadhi ya mikoa hiyo ni Shinyanga,
Arusha, Tanga Morogoro.
Aidha kwa mujibu wa sheria ya ardhi inatamka
bayana kuwa mwanamke ana haki sawa na mwanaume katika kupata, kumiliki,
kutumia na kugawa ardhi. (Kifungu 3(2) cha sheria ya ardhi na sheria ya
ardhi ya vijiji za 1999).
Hata
hivyo ni muhimu kila mmiliki wa ardhi awe na hati/ cheti halisi cha
hakimiliki kuthibithisha haki yake ya kumiliki ardhi kisheria.
Regards
Tone Multimedia Company Limited
Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street
Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania
Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892
E-Mail info@tonemg.com
Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa
EmoticonEmoticon