Kiungo mshambuliaji wa City, Ramadhani
Chombo Redondo amesema mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania dhidi ya
Simba uliopangwa kuchezwa jumapili hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
utakuwa mgumu kutokana na mazingira ya timu zote mbili.
Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo, Chombo amesema kuwa City
inakwenda Dar kucheza mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo
wa uliopita kama ilivyo kwa simba, jambo ambalo linaufanya mchezo huo
kuwa mgumu kutokana na uhitaji wa matokeo kwa timu zote.
“Ni wazi utakuwa mgumu, hii ni kwa sababu kila timu
inahitaji matokeo baada ya kupoteza mchezo uliopita,Simba na timu nzuri
na wako kwenye nafasi nzuri pia lakini wasitegeme kupata ushindi kw
sababu sisi tunauhitaji zaidi yao” alisema.
Aidha Chombo aliweka wazi kuwa City ina nafasi kubwa ya kufanya
vizuri kwenye mchezo huo hasa ukizingatia kuwa imekuwa na historia
nzuri kila inapokutana na Simba kwenye uwanja wa Taifa.
“City imeshinda mara kadhaa mbele ya Simba,hili ni jambo
nzuri kisaikolojia kwa sababu linaleta kujiamini,imani yangu kubwa
dakika 90 za jumapili zitakuwa upande wetu” alisema.
Kuhusu ligi kuu ya Vodacom inayoendelea sasa Redondo aliweka wazi
kuwa imekuwa ngumu na yenye changamoto nyingi sana,hasa ukizingatia kuwa
timu nyingi zilijiandaa vizuri toka mwanzo wa msimu ingawa pia suala la
kusima simama au kupanguliwa kwa ratiba linapunguza msisimko wake.
EmoticonEmoticon