“UKAGUZI WA VYOMBO MAJINI KUHAKIKISHA UBORA NA USALAMA”

February 17, 2016
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa nchi kavu na Majini Mkoani Tanga (Sumatra) wakishirikiana na Jeshi la Polisi kikosi cha Maji mkoani hapa wameanza ukaguzi maalumu wa siku saba kwa vyombo vya majini ili kudhibiti ubora na usalama kitendo ambacho kitasaidia pia kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na ubovu kwa baadhi yao.

Zoezi hilo litasimamiwa na Afisa mfawidhi wa SUMATRA Tanga Dr.
  Walukani Luhamba, Maafisa wakaguzi wa vyombo vya majini Captain Alex Katama, Mhandisi Christopher Mlelwa waliotokea makao makuu.

Akizungumza na Tanga Raha Blog, Ofisa Mfawidhi wa Sumatra mkoani Tanga, Dkt Walukani
  Luhamba alisema hali hiyo itasaidia pia kudhibiti wimbi la uingizwaji wa madawa ya kulevya unaopitishwa na vyombo ikiwemo ubora wa vifaa vya
usalama na kuhakikisha vinafanya kazi kwa mujibu wa sheria na
vitakavyobainika kukiuka viwango vya ubora kisheria kuzuiwa kufanya
kazi.

Alisema sambamba na hilo itasaidia kuvifanya vyombo vinavyofanya
  biashara zisizokuwa halali kuhofia iwapo vitafanya hivyo vitakumbana na adhabu kali ikiwemo kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria zilizopo. 

Vyombo visivyosajiliwa na Sumatra vitachukuliwa hatuaya kisheria ikiwa ni pamoja na faini ya shilingi 500,000/= au faini
pamoja na kifungo kulingana na sheria. (Merchant shipping act 2003)
   “Mara nyingi vyombo ambavyo vinafanya kazi zao majini hasa katika bandari bubu visivyokuwa na leseni vimekuwa vikijihusisha na uingizaji wa madawa ya kulevya hivyo ukaguzi huu utawezesha kusaidia kupunguza wimbi la uingizwaji wa madawa ya kulevya kupitia bandari hizo “Alisema Dkt Luhamba.

Aidha alisema kuwa ukaguzi huo utakwenda sambamba na kutoa elimu kwa
  wamiliki na watumiaji ikiwemo kuangalia kama wamiliki wa vyombo vya majini wanafuata sheria za majini kama ilivyoelekezwa.
  “Unajua sheria ya udhibiti wa vyombo vya majini (Merchant Shipping Act, 2003 inayoelekeza vyombo vyote vya usafirishaji majini lazima vikaguliwe na kusajiliwa kupitia mamlaka husika Sumatra “Alisema Dkt Walukani.

“Lakini vitu vya kuzingatia kabla ya chombo kusajiliwa ni kwanza

kinatakiwa kukaguliwa sambamba na kuwepo kwa vifaa vya kujiokolea, kiwe na Nanga na Injini kwa ajili ya kuendesha shughuli zao “Alisema
 
Alisema kuwa ukaguzi huo wa mara kwa mara licha ya kusaidia kupunguza  ajali lakini pia utawezesha kuondoa ongozeko la uingizaji wa madawa ya kulevya mkoani Tanga kwa sababu baadhi ya waingizaji wa bidhaa hizo wanatumia bandari bubu zilizopo kufanya biashara hizo.

Hata hivyo aliwataka wananchi waliopo maeneo mbalimbali mkoani hapa
  kutoa ushirikiano kwa maafisa wa Sumatra watakaokuwa wakipita kwenye maeneo yao kwa ajili ya kaguzi hizo zenye lengo la kukabiliana na hali hiyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »