Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa amesema wagonjwa wapatao 6,846 wamepata huduma za Afya Katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni tangu ilipokamilika na kuanza kutoa huduma.
Amesema ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu jumla ya shilingi Bilioni 7.3 ambapo Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 4.3 na wadau wa Islamic Help wametoa kiasi cha shilingi Bilioni 3.
Amesem mpaka sasa jumla ya majengo yaliyokamilika ni 15 amesema Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga hadi sasa imeshapokea wajawazito 900 na kati yao 300 walijifungua kwa njia ya upasuaji ndani ya miaka mitatu(3).
Rais Samia amefanya uzinduzi wa hospitali hiyo akiwa katika ziara mkoani Tanga ambayo ameanza leo Februari 23, 2025 hadi Machi 1, 2025 kwa lengo la kukagua na kuzindua miradi mbaliambali iliyotolewa fedha na Serikali.
EmoticonEmoticon