Tigo yaomba wateja wake radhi kwa kukatika kwa huduma zake

November 09, 2015


Dar es Salaam, Novemba 09, 2015: Kampuni ya simu ya Tigo imeomba radhi wateja wake kutokana na kukatika kwa huduma zake katika sehemu nyingine nchini jana.

Taarifa ya kampuni hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam imesema kukatika kwa huduma za Tigo “kulitokana na sababu zilizo nje ya uwezo kwa kampuni zilizo tokana na kukatika kwa mkongo sehemu tofauti tofauti.” Aidha taarifa hiyo iliendelea kusema kwamba “tatizo hilo sasa limeshughulikiwa kikamilifu na huduma zote za Tigo zimerejea katika hali yake ya kawaida.’’

“Tuna sikitishwa na usumbufu uliojitokeza kutokana na kukatika kwa huduma zetu natunapenda kuwahakikishia wateja wetu dhamira ya kampuni yetu kuendelea kuwapa wateja huduma zenye ubora wa hali ya juu, za kutegemewa na kwa gharama nafuu,” amesema Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez.


Aidha Gutierrez ametoa shukrani kwa wateja wa Tigo kwa uvumilivu wao na kutangaza kwamba kama ishara ya kuomba msamaha kampuni ina wapa wateja wake wote dakika 10 za muda wa maongezi, SMS za bure kwenda mtandao yote na 10mb za kuperuzi Intaneti kwa siku nzima ya leo.Kifurushi hiki mteja ana kipata kwa kutuma neno BURE kwenda namba 15304.

Mwisho

Kuhusu Tigo:
Tigo ni kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi yenye ubunifu mkubwa nchini Tanzania , ikijulikana kama “nembo ya maisha ya kidijitale yanayojitosheleza”. Inatoa huduma mbalimbali kuanzia huduma ya sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha za kwenye mitandao ya simu za mikononi, Tigo imeanzisha ubunifu kama vile Facebook ya Kiswahili, Kiunga cha Tigo Pesa kwa watumiaji wa simu za Android & iOS, Tigo Music( Deezer)na huduma ya kwanza Afrika Mashariki kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika.

Intaneti ya Tigo ya 3G inatoa huduma bora kwa wateja wake katika mikoa yote nchi nzima, na hivi karibuni tumezindua mtandao wa 4G ambao kwa sasa unapatikana Dar es Salaam nzima,na tunatarajia kuzindua nchi nzima. Kati ya mwaka 2013 na mwaka 2014 pekee kampuni ilizindua zaidi ya maeneo mapya 500 yenye mtandao wa Tigo na kufanya kuwa zaidi ya maeneo 2000 ya mtandao na inapanga kuongeza uwekezaji wake mara mbili ifikapo 2017 katika suala la upatikanaji wa mtandao na kuongeza uwezo wa upatikanaji wa mtandao kwa maeneo yasiyofikika kabisa vijijini. Pamoja na kuwa na zaidi ya wateja milioni 9 waliosajiliwa, Tigo imeajiri zaidi ya watanzania 300,000 ikiwa ni pamoja na mtandao wa wawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha za kwenye simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.
Tigo ni nembo kubwa ya kibiashara ya kampuni la Millicom, kampuni ya kimataifa inayoendeleza maisha ya kidijitale katika nchi 11 pamoja na shughuli za kibiashara katika Afrika na amerika ya Kusini na ina ofisi kubwa Ulaya na Marekani. Pamoja na ujuzi Fulani walionao ambao unawafanya kubuni mara kwa mara na kuwafanya wawe juu, Millicom anaendelea kujenga thamani kubwa kwa mbia; kutumia dhana yao ya "mahitaji zaidi"  hivi ndivyo wanafanya biashara na kurejesha nafasi yao kama viongozi wa maisha ya kidijitale hasa katika masoko zaidi ya kipekee na yenye changamoto.



Kwa taarifa zaidi tembelea:  www.tigo.co.tz au wasiliana na:
John Wanyancha – Meneja Mawasiliano

Wasaaalam photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »