Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi
amewatumia salamu za pongezi wachezaji Mbwana Samatta na Thomas
Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Congo DR kufuatia kutwaa
Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) jana kwa kuifunga timu ya USM
Algiers kwa jumla ya mabao 4-1.
Katika salamu zake kwenda kwa wachezaji hao, Malinzi amewapa hongera
kwa mafanikio waliyofikia ya kutwaa ubingwa huo wa vilabu Afrika, na
kuwataka waongeze bidii ili waweze kufanya vizuri pia katika michuano ya
Kombe la Dunia la Mabara litakalofanyika mwezi Disemba nchini Japan.
Malinzi amesema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu na Watanzania
wote wanawashukuru kwa kuiwakilisha vizuri Tanzania kimataifa, na sasa
moyo huyo wa kujituma kwao waundeleleze katika mchezo dhidi ya Algeria
wikiendi hii kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia 2018 nchini
Urusi.
EmoticonEmoticon